jamii
TAARIFA MAALUM
Habari ya muda huu family members,
TANGAZO
Napenda mfahamu kuwa mchakato wa kufungua account ya Azania alumni 2000 unaendelea, japokuwa tumekuwa tukipata ugumu kutokana na kushindwa kupata nafasi ya pamoja ya kufika pale branch kwa sisi watia sahihi, na hii ni kutokana na dharula za kiofisi na majukumu yake.
Lakini mpaka kufikia siku ya ijumaa wiki hii tutakuwa tumemaliza zoezi hilo.
Na pia napenda mfahamu kuwa imetubidi kumuondoa kwa idhini yake mwenyewe, mwenyekiti wa kamati ya uchumi na mipango ndugu Joseph Mwaisemba kwenye nafasi ya watia sahihi wa account kutokana na kuwepo kwake nje ya mkoa wa Dar es salaam kwa shughuli za kikazi, na nafasi hiyo tukamuweka katibu wake ambaye ni Francis Ambali.
Na pia tumepunguza mtia sahihi mmoja kila group (yani group A, na group B) kutokana na mahitaji ya taratibu za benki ya Posta, ya kuhitaji watia sahihi wawili kila kundi, na kufanya idadi ya watia sahihi kuwa ya watu wanne tu, badala ya sita tuliowachagua kwenye mkutano mkuu wa tarehe 31 May.
Hivyo tumebaki na watia sahihi wafuatao.
Group A
1. Mwenyekiti Azania Alumni 2000 ndugu Mwinyi Hassan.
2. Mweka hazina ndugu Ntimi Omega Mwakipake.
Group B
1. Katibu kamati ya Uchumi na Mipango ndugu Francis Ambali.
2. Mjumbe kamati ya Uchumi na Mipango ndugu Issa Massoud.
Ahsanteni sana
Mwinyi Hassan
Mwenyekiti Azania Alumni 2000.
0 comments: