Showing posts with label Uchumi. Show all posts

RATIBA KAMILI YA MKUTANO MKUU WA UCHUMI JUMAMOSI DON SUITE




RATIBA YA MKUTANO MKUU WA UWEKEZAJI. 9/01/2016 UTAKAO FANYIKA KTK UKUMBI WA DON SUITE HOTEL


SAA 5:00 MPAKA SAA 6:00 MCHANA.
Usomwaji wa taarifa ya manunuzi ya shamba la Fukayosi, na taarifa ya hali ya fedha katika account ya TPB. Pamoja na uwezekano wa kununua shamba jingine.

SAA 6 MPAKA SAA 7 MCHANA:
Majadiliano/Hatua za kufanya juu ya uanzishwaji wa Saccoss.

SAA 7 MPAKA SAA 7.45 CHAKULA CHA MCHANA.

SAA 7:45 MPAKA SAA 8:45. MCHANA.
Uanzishwaji wa  kampuni/ Uteuzi wa Board of Directors/ Mchanganuo wa ununuzi na umiliki wa share katika kampuni.

SAA 8:45 MPAKA SAA 9:00 ALASIRI MENGINEYO.

SAA 9:00 KUFUNGA MKUTANO.⁠⁠⁠⁠

BY DOLF GERLAD



FUKAYOSI : TUMAINI JIPYA KWA WENYE NIA YA KWELI AZANIAALUMNI





Kila penye nia pana njia ndio kauli pekee ifaayo kuanza nayo, ama kwa hakika FUKAYOSI naweza kusema ndio tumaini jpya kwa wana Azaniaalumni wenye nia ya kweli ya kutaka kusonga mbele kimaendeleo, kila jambo la maendeleo linahitaji juhudi na kujitolea ili liweze kufanikiwa napenda kuwashukuru wana Azaniaalumni wote waliokuwa na nia ya kweli katika kujikwamua kiuchumi na kuwezesha kupiga hatua hii.


kutoka kushoto ni Said Mselem, Francis Ambali, Godfrey Lutare, Mwinyi Hassani ( Mwenyekiti- AzaniaaLumni2000) na Simon Matere ( Katibu-Azaniaalumni2000)  wakikagua shamba la FUKAYOSI Mjini Bagamoyo


timu ya awali iliyokwenda kufanikisha umiliki wa shamba la FUKAYOSI kutoka Kushoto ni Issa Masoud, Joseph Mwaisemba( Mwenyekiti kamati ya Uchumi) Simon Matere ( Katibu-AA200)  Hilorims Mayombo, Mwinyi Hassani ( M/Kiti-AA2000) na Dr. Ramadhan Idd


Mwenyekiti wa Uchumi Ndugu Joseph Mwaisemba akitia saini  hati ya Kijiji kukamilisha ununuzi wa shamba hilo.

Ikawa zamu ya Mwenyekiti wa AA2000 Ndugu Mwinyi Hassani kuweka ushahidi wake wa kimaandishi.

Deal Done!!!! Mmiliki wa shamba akitia saini ya dole gumba kukubali kuamisha umiliki wa shamba lake kwenda kwa wana AA2000



Money Make the World go round!!! zoezi likahitimishwa kwa makabidhiano ya kiasi cha fedha kilichokubaliana mbele ya serikali ya mtaa


Ikafika zamu ya wawakilishi wetu kukabidhiwa shamba kwa kuoneshwa mipaka stahili, na hapo tumaini jipya likafufuka, 

FUKAYOSI ndio yetu MOSI ...........

Mengi twatumaini..........

KILA LA KHERI SAFARINI BAGAMOYO


TAARIFA!

Kwa niaba ya Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi na Mipango, ndugu Mwaisemba. Kamati inapenda kuwajulisha wanachama wote wa AA2K kua ile safari ya kwenda Bagamoyo kutafuta maeneo itafanyika siku ya Jpili  tarehe 15 Nov 2015. Safari hii ilichelewa kidogo kupisha maswala mazima ya uchaguzi wa nchi yetu. Uongozi wa kamati umeteua wajumbe wafuatao watakao tuwakilisha katika safari hiyo. 

1. Ndg, Joseph Mwaisemba-Mwenyekiti wa kamati.
2.Ndg, Mwinyi Hassan- Mwenyekiti AA2K 
3.Ndg, Simon Swai- Katibu mkuu AA2K 
4.Ndg, Francis Ambali - Mwenyekiti Kamati ya mambo ya Jamii.


Ndugu watajwa hapo juu tafadhari mnaombwa mtoe ushirikiano wenu wa hari na mali kuweza kufanikisha safari hiyo. Uongozi wa kamati ya uchumi na mipango unawatakia safari njema na mafanikio tele. Ieleweke kwamba mioyo macho na masikio yetu wote wana AA2K yatakua pamoja nanyi. Aidha kamati inaendelea kusisitiza kwa wadau wote kutosubiri mpaka june 2016 bali tuendelee kuchanga kidogo kidogo ili kuweza kukabiliana na fursa yoyote itayojitokeza hivi karibuni. Pia Kamati inapenda kuweka bayana na kudhihirsha kwamba hii ni mipango ya UCHUMI wa wana Azania Alumni 2000. Idadi ya waliochanga mpaka sasa ipo na wanafahamika kwa majina, kwa hiyo fursa itapo jitokeza yule aliye/ atakae changia ndiye atakae faidika nayo. Mungu ibariki Tanzania Mungu ibariki Azania alumni 2000. 

Asanteni Adolph Gerald Katibu - Kamati ya Uchumi na Mipango AA2K.

MWANA AZAPOUND NIMEKULETEA LIST ZA BIASHARA MBALIMBALI..KAMATA MOJA TWENZETUU


Mwana Azanialumni2000 wengi huumiza vichwa kutafuta Business Idea kwa ajili ya kuanzisha biashara leo NIMEKULETEA LISTI YA FURSA ZA BIASHARA NA MIRADI MBALIMBALI kaa chini set your goal weka nia anza safari sasa,

1. Kununua Mashine za kukoroga zege na kukodisha. 
2. Kununua Mashine za kukata vyuma na kuzikodisha.
3. Kutengeneza na kuuza tofali 
4. Ufundi, Website updating/Database: Katika Halmashauri, Manispaa, Mashule, Wizara, Wilaya na Makampuni mbalimbali. 
5. Kuanzisha kituo cha redio na televisheni 
6. Kufunga na kutengeneza vifaa mbalimbali vya electroniki na mawasiliano mfano; compyuta na vifaa vya compyuta na mawasiliano. 
7. Kuuza software; mfano Antivirus, Operating Systems, Pastel, Tally, Myob, n.k 
8. Kushona na kuuza nguo.
9. Kufungua Duka la kuuza nguo mpya; suit, socks, batiki, nguo za asili, Mashuka, Mashati, Suruali, 10. Ufugaji wa mifugo mbalimbali mfano Kondoo, Mbuzi, Ng’ombe, Kuku, Bata, na wengine. 
11. Kufungua stationery, kuuza (supply) vitabu na vifaa mbalimbali ktk mashule na vyuo. 
12. Kutoa ushauri mbalimbali wa Kitaalamu.
13. Kuuza viazi, mahindi, mihogo, kutengeneza popcorn na kuziuza. 
14. Kusajili namba za simu na kuuza vocha 
15. Kuwa na mradi wa Pikipiki zisizotumia mafuta na zinazotumia mafuta 
16. Kilimo cha mazao mbalimbali kulingana na hali ya hewa ya sehemu husika. 
17. Kuuza Mitumba 
18. Kusimamia miradi mbalimbali 
19. Kufungua duka la kuuza mitambo mbalimbali 
20. Kufungua banda la chakula na chips 
21. Kukodisha turubai viti na meza 
22. Kufungua Supermarket 
23. Kufungua Saluni 
24. Kufungua Bucha 
25. Video Shooting & Editing. 
26. Kufungua Internet cafe 2
7. Duka la kuuza matunda 
28. Kufungua duka la kuuza vifaa vya simu za mkononi na landline.
29. Kufungua duka la vifaa vya ujenzi; cement, vifaa vya umeme, duka la mabati 
30. Kutengeneza michoro mbalimbali ya majumba na miradi ya ICT 
31. Kuchapa vitabu, bronchures, n.k 
32. Kuanzisha kampuni ya ujenzi (Building contractor) 
33. Kuuza Vifaa vya umeme wa nishati ya jua (solar) ,battery, inverter na vifaa vingine vya solar n.k 34. ** Kuuza maji kwa jumla na rejaleja. 
35. Kutengeneza na kuuza Unga wa lishe bora. 
36. Kukodisha Music 
37. Kuanzisha Mradi wa Taxi 
38. Kuanzisha mradi wa Daladala 
39. Kuuza vifaa vya Kompyuta, laptops, converters, HDDs, Monitors, Softwares, CD Copiers na vifaa vingine. 
40. Kununua magenerator na kukodisha 
41. Kufungua kampuni ya kutoa huduma za simu 
42. Kufungua kampuni ya kutoa huduma za internet (ISP) 
43. Kuuza mabati na vigae 
44. Kujenga apartments 
45. Kufungua Kisima cha mafuta ya taa au mafuta ya aina zote 
46. Kufungua Duka la samaki 
47. Kufungua Duka la nafaka 
48. Kufungua Shule za Awali, Shule za Msingi, Sekondari na Vyuo. 
49. Kujenga hostel 
50. Kuuza vocha na ving’amuzi vya DStv, Zuku, Startimes, Easy TV, TNG, Digitech, Continental. 51. ** · Kujenga mtambo wa kuzalisha umeme na kuuza katika viwanda na wananchi. 


52. Ufundi simu 
53. Kufungua Hospitali, Zahanati. 
54. Maabara ya Macho, Meno 
55. ** Kuchimba/Kuuza Madini 
56. ** Kufungua ofisi ya kutoa huduma ya simu na fax 
57. Kuuza miti na mbao 
58. Kufungua Grocery 
59. Kufungua studio ya kupiga na kusafisha picha 
60. ** Kucharge simu/battery 
61. Duka la TV na vifaa vingine 
62. Kuanzisha biashara ya kuuza vyakula katika sherehe na tamasha mbalimbali (catering). 
63. Banda la kupigisha simu 
64. Kuuza na kushona Uniform za shule 
65. Kuanzisha duka la kuuza vitu kwa jumla.
 66. Kufungua gereji za kutengeneza bajaji, pikipiki na magari 
67. Kuuza vyuma, pembejeo, rake, jembe 68. Kuuza fanicha 
69. Kufungua sehemu ya kuziba pancha za matairi ya magari na mitambo. 
70. Kujenga nyumba za kulala wageni (hotel) 71. Kuagiza na kuuza vifaa vya aluminium. 
72. Kuuza vioo 
73. Kushona na kukodisha nguo za harusi 
74. Kufungua yard kwa ajili ya kuosha magari 
75. Kuuza mashine za kuchomelea (welding machine). 
76. Kuuza vifaa vya kuvaa Site (boots, helmets etc) 
77. Kununua mabasi kwa ajili ya kusafirisha wanafunzi 
78. Kufungua studio ya kutengeneza vipindi vya redio na televisheni 
79. Kuanzisha ofisi ya michezo ya televisheni (TV Games) 
80. Kufungua benki 81. Kuwa na malori ya kubeba kokoto na mchanga 
82. Kuuza vifaa mfano TV, CCTV Camera, n.k 
83. Kuwa dalali wa vitu mbalimbali 
84. Kuanzisha mradi wa kukodisha fork lift na winchi (crane) 
85. Kuanzisha kiwanda cha kutengeneza viatu. 
86. Kuanzisha viwanda mbalimbali 
87. Duka la vifaa vya simu na gadgets mbalimbali zinazoendana na mawasiliano ya Vodacom, TTCL, AIRTEL, TIGO, ZANTEL, n.k. 
88. Kujenga Ukumbi wa kukodisha kwa sherehe, mikutano mbalimbali 
89. Kununua matrekta, mitambo ya ujenzi wa barabara na kukodisha 
90. Kutengeneza antenna na kuuza 
91. Kufungua mradi wa Machine za kusafisha, kutoboa na kuchana mbao 
92. Kufungua mradi wa kuuza vifaa vya Umeme wa kutumia upepo 
93. Biashara ya kuagiza magari 
94. Kufanya biashara za Jukebox 
95. Kukodisha matenki ya maji** 
96. Kufungua duka la kuuza Asali 
97. Kutengeneza Mikokoteni/ matoroli na kuikodisha 
98. Kufungua Duka la vinyago, batiki 
99. Kuanzisha huduma ya AIRTEL MONEY, MPESA, TIGOPESA, EZY PESA 
100.Kuanzisha sehemu ya kufanyia mazoezi (Gym). 
101. Kununua na kuuza vifaa vya kupima ardhi. 
102. Kufungua duka la kuuza dawa (pharmacy). 
103. Kufungua Kampuni ya Ulinzi 
104. Kufungua kampuni ya "Clearing and fowarding" 
105. Kuchezesha vikaragosi 
106. Kuuza spea za bajaji, magari na pikipiki 
107. Kuuza baiskeli 
108. Kuuza magodoro 
109. Kuuza vyombo mbalimbali kwa ajili ya matumizi ya nyumbani mfano bakuli, sahani, vikombe, vijiko, 
110. Kuuza marumaru (limestones) 
111. Kuuza kokoto 
112. Kuuza mchanga 
113. Kufundisha Tuisheni 
114. Biashara za bima 
115. Kampuni ya kusafirisha abiria kwa njia ya anga (ndege) 
116. Biashara za kitalii 
117. Biashara za meli na maboti. 
118. Kampuni ya kuchimba visima 
119. Kufungua ofisi ya wakili/mawakili wa kujitegemea 
120. Kuuza mkaa 
121. Kutengeneza mashine za kutengeneza tofali 
122. Kampuni ya kupima ardhi 
123. Kampuni ya magazeti 
124. Kuchapa (printing) magazeti 
125. Kuuza magazeti
126. Kuchimba mafuta 
127. Kiwanda cha kutengeneza mabati 
128. Kiwanda cha kutengeneza fanicha 
129. Kiwanda cha kutengeneza matairi 
130. Kutengeneza vitanda vya chuma 
131. Kununua nyumba katika Maghorofa (Apartments) na kuzikodisha. 
132. Kukodisha makapeti 
133. Kupamba maharusi na kumbi za harusi/sherehe. 
134. Mashine ya kusaga na kukoboa nafaka. 
135. Kazi ya ususi na kusafisha kucha. 
136. Kuuza Gypsum 
137. Malori ya kubeba mafuta na Mizigo 
138. Duka la kuuza mboga za majani 
139. Duka la kuuza maua. 
140. Kampuni ya kuzoa takataka 
141. Kampuni ya kuuza magari 
142. Kuuza viwanja 
143. Uvuvi 
144. Kutengeneza na kuuza nguzo za kujengea fensi 
145. Uchoraji wa mabango. 
146. Duka la kuuza silaha 
147. Ukumbi wa kuonesha mpira 
148. Biashara ya mlm (network marketing) 
149. Yadi kwa ajili ya kupaki magari 
150. Mradi wa trekta za kukodisha kwa ajili ya kilimo


KAMA YOTE HAYA UMESHINDWA KUPATA LA KUFANYA, MWANA AZAPOUND BASI TUENDELEE KUWA WAAJILIWA WA SERIKALI NA TUSUBILI KUSTAAFU TU.

BONDE LA MTO PANGANI LAVAMIWA SERIKALI YATOA ONYO KALI!!!


Kati hali inayopelekea kuhatarisha uhai wa mto Pangani kufuatia wavamizi waliojitokeza kando kando ya mto huo ambao wanaendesha shughuli za kilimo na wengine kudiriki kuchimba mabwawa makubwa kwa ajili ya ufugaji samaki kinyume na taratibu za hifadhi za mto huo, Serikali imetoa onyo kali na kuahidi kuwachukulia hatua kali wale wote watakaobainika kuendesha shughuli kinyume na hifadhi za mto Pangani, Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja Wizara ya Nishati na Madini zinavyosema.


Meneja wa Tanesco vituo vya umeme vya  Hane , Nyumba ya Mungu na Pangani Mhandisi John Skauti akizungumza kupitia kituo cha TV cha  Channel Ten amesema kina cha maji katika bwawa la Nyumba ya mungu kinazidi kupungua siku hadi siku kutokana na Mabepari hao waliojitokeza kando kando ya mto na kuitaka serikali kuchukua juhudi za haraka kupambana na Ujangiri huo mara moja hali inayopelekea kuhatarisha uzalishaji wa umeme katika kituo hicho kupungua kutoka Mega Watts 100 hadi 24 kitu kinachopelekea kuliingiza Taifa gizani bila sababu za msingi.



Afisa Msimamzi wa Bonde la Mto Pangani Bwana Vanderine Baso anayeshughulikia matumizi ya maji ya mto Pangani naye ameitaka Serikali kuwachukulia hatua kali wale wote walio kando kando ya mto huo na wenye matumzi makubwa kupita kiwango ambao wanahatarisha uhai wa Mto Pangani watafutwe na wafikishwe sehemu husika kama itabahinika wanafanya shughuli hizo kinyume na taratibu.

Ushauri kwa Viongozi na Azaniaalumni 2000 kuachana na michakato iliyokuwa inaendelea ya kununua Ardhi Pembezoni mwa Mto huo kusitishwa mara moja kwani hali halisi ya Bonde hilo imeshaanza kutia mashaka kufuatia onyo hilo kutoka mamlaka husika.

AZANIAALUMNI2000 FOREVER!!!!!!!!!!!!!!!!

PANGANI KULALA NA NJAA KUPENDA


"Pangani kulala na njaa kupenda " ndio kauli mbio yetu sote, twende Pangani, wana Azaniaalumni tunaombwa kutupia mchango wa kukuza uchumi kiasi chochote kile ulicho jaaliwa ili kutimiza adhima ya kujiinua kiuchumi ili tuweze kununua Ardhi iliyopo pangani yenye ukubwa wa ekari 33 kwa gharama ya Tsh 20M.



 Kwa mujibu wa timu iliyotembelea eneo hilo ndugu Ntimi Mwakipake, Mwinyi Hassani,  Ayubu Misheli na Allan Rwechungura eneo hilo ni HOT CAKE  lenye rutuba tele na lililo  pembezoni mwa mto Pangani ,eneo lina hati miliki zote za kiserikali na linafikika kwa njia zote za usafiri, TUPIA TPB  TWENDE PANGANI.



Eneo hilo pia limepakana na Shamba kubwa la Bepari mmoja aliyebobea kwenye kilimo cha umwagiliaji wa kisasa kitu ambacho kitaleta changamoto za kupata ujuzi kama Azaniaalumni wataamua kuwekeza kwenye kilimo, vilevile eneo linafaa kwa uwekezaji wa ufugaji wa samaki kitu ambacho Azania alumni wanajivunia kuwa na Mtaalam wa Ufugaji Afrika Mashariki ndugu Ayubu Misheli.


JE ni nani tunayemtaka aje ili atuwezeshe kulichukua eneo hilo potential kwa faida zetu kama sio sisi wenyewe wana AZAPOUND?

"TUPIA TPB TWENDE PANGANI"

FAHAMU YALIOJIRI MJADALA WA UCHUMI...SACCOS VS ARDHI UWEKEZAJI


Kamati ya Uchumi na Maendeleo ya Azaniaalumni 2000 tar 02/10/15 hadi 03/10/15 iliendesha Online Meeting kwa siku mbili kupitia Whatsapp kuhusiana na uwekezaji, Agenda kuu ilikuwa ni kujadili kipi kati ya SACCOS na ARDHI kipewe kipaumbele katika hatua hizi za mwanzo za Azaniaalumni 2000 katika kujikwamua kiuchumi.

Mjadala ulikuwa mkali sana wajumbe walipata nafasi ya kutoa mawazo yao kuhusu Ajenda  hiyo, wapo waliosema SACCOS ndio kimbilio la wengi na baadhi wakisema ARDHI ni madini yasio oza ama kwa hakika mjadala ulileta changamoto kubwa.





Majibu ya Mjadala huo kipi kianze kati ya SACCOS au ARDHI ama vyote kwa pamoja utaamuliwa na kamati ya Uchumi na Maendeleo baada ya kukaa na kujadili kwa kina mapendekezo ya wajumbe wote waliochangia. Usipitwe na majibu hayo endelea kutembelea www.azaniaalumni2000.blogspot.com kwa habari zaidi.

KWAKO MWANA AZAPOUND


"TPB ndio mpango" hii ndio kauli mbio ya sasa, ewe mwana  Azapound popote ulipo kamilisha lile adhimio lililowekwa kwa kutupia mkwanja kwenye bank kongwe ya Posta kila mwezi ili kufikia lengo letu la kumiliki Ardhi, Tupia 85,000/- au na zaidi kwa muda usiozidi mwaka moja ili tuwape ulithi wale watakaokuja.

Tuache  kuchungulia makaratasi haya,Thamani yake uonekana kwa kile ulichoekeza.

TPB NDIO MPANGOOOOOOOOOOOOO!!!!!!


KWAKO MWANA AZANIAALUMNI2000


Mwana Azapound unakumbushwa kuanza kuwekeza Fedha kama maazimio ya uwekezaji katika ardhi yalivyofikiwa hapo awali,unahimizwa kutekeleza adhimio hilo ili kuendana na muda uliopangwa kutoa kwako kwa wakati ndio mafanikio ya maadhimio hayo. 

Taarifa na mahali pakupeleka Fedha hizo ni Post Bankkupitia  AZANIA ALUMNI 2000 A/c no: 111-00000367 Tafadhali mara ukamilishapo uwekaji wa fedha hizo wasilisha stakabadhi yako  kwa Muweka Hazina wa Azaniaalumni200 ndugu Ntimi Mwakipake.



TUWEKEZE KWA FAIDA YETU NA VIZAZI VIJAVYO. 

TAARIFA TAARIFA

Wana wa azaniaalumni2000  mnaombwa kuipitia nakala ya form ya usajili ya mwanachama ili kufanyiwa marekebisho inapobidi, Pia Unaombwa kutoa maoni kwa baadhi ya vipengele.

Form ya Kwanza

Form ya pili 

 Form ya Tatu

Taarifa@katibu Azaniaalumni2000
Simoni Isidory Swai

TAARIFA NJEMA





Habari ya muda huu family members.

Napenda kuwapa taarifa kuwa lile zoezi letu lililokuwa linasubiria kwa hamu, hatimae limekamilika leo. Azania Alumni 2000 imepata akaunti yake katika benki ya posta (TPB) TANZANIA POSTAL BANK, details za account ni kama ifuatavyo; A/c name: AZANIA ALUMNI 2000 A/c no: 111-00000367 Napenda nipongeze jitihada na uvumilivu wetu sote, katika kuhakikisha jambo hili linakamilika, HIZI NI SIFA ZINAZOMSTAHILI KILA MMOJA WETU. 


Ahsante sana Mwinyi Hassan,


AZAPOUND BANK ACCOUNT

Kuhusiana na kufungua akaunti,

Kama nilivyoahidi siku ya jumamosi kuwa jumatatu tungepata namba ya akaunti yetu, lakini haikuwa hvyo naomba radhi sana kwa hilo, na kwa bahati mbaya sana kibarua kikanibana, nikashindwa kufika pale tangu jumatatu, na pia sikuona simu kutoka kwao, ikanipa mashaka, kiasi cha kufanya jitihada kufika pale leo mchana.

Nilipofika nikapata kujua kuwa kuna sehemu ya katibu mkuu wa Azania alumni 2000 hapajasainiwa bado, na ni kutokana na wao kusema watafungua akaunti, atasaini baadae, lakini meneja wa tawi alitaka lazima pasainiwe ndio akaunti ifunguliwe, hvyo kesho, Katibu mkuu ndugu Simon Matere atafika pale kutia sahihi, na akaunti kufunguliwa.

Kuhusiana na swali la kaka Deo Katundabwile alilouliza leo asubuhi, je watu walio nje ya Tanzania watawezaje kuweka pesa kwenye akaunti ya kikundi wakiwa huko?, swala hilo litakuwa sio tatzo, wanaweza kuweka hela huko walipo, kwani TPB, imejiunga na Standard Chartered Bank na Bank of Baroda, ambazo zinatoa huduma kimataifa, na zina matawi  nchi nyingi, malekezo jinsi gani ya kufanya utayapata utakapofika benki zilizotajwa hapo juu.

Napenda kutoa pendekezo, wale walioweka pesa yao ya kuanza zoezi la kudeposit mwezi huu, basi wakae nazo tayari kwa kuanza kutunisha mfuko, maana zoezi linaanza rasmi mwezi, au niseme wiki hii.

Na kuhusiana na idadi gani ya wanachama walio hai, tuna wastani wa wanachama wasiozidi sabini na tano, hvyo tegemeeni mkono wa chuma kupita wiki hii ili kuziba hilo gape la wanachama wasio hai.

Hivyo basi kama kuna mtu ana namba za wana Azania alumni 2000 ambao wako tayari, na hawako humu, tafadhali tumeni namba zao inbox yangu ili niwa-add.

Ahsante sana,

Mwinyi Hassan

Mwenyekiti Azania alumni 2000.

Uchumi


Mwana Azapound kwasasa tupo kwenye mchakato wa kujikwamua kiuchumi kwa kuandaa mchakato wa kuweza kumiliki ardhi na ikiwezekana hatua zingine zaidi zifuate,Tafadhali tunahitaji mshikamnano wako thabiti.