simulizi

MFAHAMU MUANZILISHI WA AZANIAALUMNI2000

2:43 AM tibazetuasili 0 Comments


Pongezi nyingi sana zimuendee muwanzilishi wa group la azaniaalumni2000 aliyefikiria jambo kubwa sana lililoleta mshikamano mpya miongoni mwa wanafunzi wa Azania waliomaliza mwaka 2000,mshikamano ambao hivi leo kila mmoja anawuona ni wenye tija sana katika kila siku ya maisha yetu.Mshikamano uliowakutanisha vijana waliopoteana kwa takribani miaka 15 iliyopita, wengi walitamani zama hizo zijirudie na kuwa pamoja lakini wasijue ni jinsi gani wangeweza kukutana tena.

Mtu pekee aliekaa akawaza na kuumiza kichwa ni jinsi gani angeweza kufanikisha muunganiko wa zama zile zenye kila mkusanyiko wa watu mbalimbali huzuni na furaha tele na kupata jawabu ambalo hivi leo kila mmoja wetu akikaa na kutafakari kwa kina lazima atoe pongezi kwake kwa mawazo yake mazuri na maamuzi aliyoyachukua,mtu huyu si mwingine bali ni NEWTON MASUNZU.

Eng Newton Masunzu

NEWTON alibahatika kusoma darasa la form IG - II na kumalizia Form III E - IV, kwasasa ni Muhandisi Majengo na mihimili (civil & stuctural engineering ) shahada aliyoipata chuo kikuu cha Dar es salaam mwaka 2008. Azaniaalumni2000 kwa pamoja inatoa pongezi kwake kwa wazo zuri la kuwakutanisha ndugu na marafiki waliopoteana kwa muda mrefu, hakuna cha kukulipa mungu akujalie uwe na mawazo endelevu kama hayo siku zijazo.

Newton Masunzu wa kwanza kushoto akishiriki katika moja ya vikao vya azaniaalumni2000


Eng Newton Masunzu katikati akiwa na Dr Abdi Msangi na Ally Lota, walipokutana baada ya kupotezana kwa muda mrefu





You Might Also Like

0 comments: