Showing posts with label michezo. Show all posts

BONANZA LA WATANI WA JADI SIMBA NA YANGA LANUKIA


Hayawi hayawi sasa yamekuwa ule mpambano wa soka kati ya mashabiki wa Simba na Yanga kutoka Azapound Family umeiva, baada ya tambo zinazoendelea kuzidi na kupelekea ubishi huo kwenda kuamulia uwanjani. Mashabiki hao wa timu mbili wamemuomba Mwenyekiti wa AzaniaAlumni Ndugu Mwinyi Hassani kuandaa mpambano huo kabla ya mwezi mtukufu wa Ramadhani ili kumaliza ubishi huo.




Mpaka sasa tayari wameshajitokeza baadhi ya member wakithibitisha ushiriki wao katika mtanange huo, Diaz Batholomeo yeye amesema yeye atawakilisha upande wa Yanga kama Golikipa na Omar yeye amesema yupo neutral ni mchezaji huru upande wowote ukimuhitaji atauchezea.

Kwa upande wa wanazi wa Yanga wakiongozwa na Katibu wa Azananiaalumni2000 ndugu Simoni Matere wamemwambia Diaz licha ya kuonyesha mapenzi yake kwa Mabingwa hao wa Bara msimu huu hawatakuwa tayari kumruhusu kukaa golini kwani imeonekana ni mamluki wa Simba anayetaka kuipa ushindi timu yake kijanja, na kumtaka akae mbali kabisa na kama ikiwezekana aende kuungana na mashabiki wenzie kuomboleza msiba wa timu yake, kwa kukosa ubingwa na kuendelea kubakia kushiriki makombe ya Mbuzi ( Mchangani ).

Ama kwa hakika terehe hiyo inasubiliwa kwa hamu kubwa sana ili kuona ni nani atakaye ibuka mshindi siku hiyo.

HIKI NDICHO KILICHOWAPATA CHELSEA NA LIVERPOOL ..NI HURUMA




Alikuwa ni Steven Naismith aliyepeleka kilio cha pili mfululizo kwa mashabaki wa timu ya chelsea pale alipofunga hat trick na kuiwezesha timu yake ya Everton kuondoka na ushindi mnono wamabao 3 kwa nunge.

Naismith alianza kupigilia Misumari hiyo ya moto kunako dakika ya 17, 22 na kumalizia Msumari wa mwisho katika dakika ya 82, hiki kinakuwa ni kipigo cha kwanza takatifu kwa chelsea kutoka kwa Everton toka msimu wa mwaka 1988-89.

Goli la kufutia machozi la The Blues lilifungwa na Nemanja Matic katika dakika ya 36 ya kipindi cha kwanza ya mchezo huo.

Katika Mchezo mwingine uliowakutanisha watani wa jadi Mashetani Wekundu  Manchester United na Majogoo wa London Liverpool, Mchezo huo uliisha kwa Man U kuchomoza na ushindi mnono wa Magoli 3-1
Alikuwa ni Daley Blind aliyeanza kuandika bao la kwanza katika dakika ya 49 na kisha Andrew Herrera kuandika bao la pili kwa Mkwaju wa penati baada ya mlinzi kinda Gomez  wa Liverpool kumshezea madhambi Herrera dakika ya 70.



Christian Benteke alifanikiwa kuifungia timu yake bao la kufutia machozi kwa tik tak kali iliyomuacha mlinda mlango David de Gea asijue la kufanya.

Alikuwa ni Anthony Martial dakika ya 86 alipowanyonyoa manyoa yote Majogoo ya London baada ya kupigilia msumari wa moto na mwisho na kuifanya Man U kuibuka kidedea kwa Jumla ya Magoli 3 -1


PATA MATOKEO YA MECHI ZA EPL WIKIENDI HII





EPL iliendelea jana jumamosi na leo kwa kuzikutanisha timu mbalimbali katika muendelezo wa ligi hiyo matokeo ya mechi za jana na leo yalikuwa ni kama ifuatavyo:-




Sunday 23rd August 2015

BARCLAYS PREMIER LEAGUE
Show last 5 matches and coverageFixtureKick-offStatus
Full time
Full time
Full time







PEDRO ATUA RASMI CHELSEA BADALA YA MAN UTD


"Maisha bila fitina hayaendi" kauli wapendayo kuitumia vijana wengi wa  kisasa, kauli hiyo imedhihirika masaa machache yaliopita baada ya Club ya Chelsea  kufanikiwa kuinasa sahihi ya  mchezaji wa Barcelona Pedro Rodriguez, 28 kwa ada ya Euro M30 na kuwaacha mashabiki wa Manchester United midomo wazi wasijue sintofahamu hiyo ama unaweza kusema wamenyan'gwa tonge mdomoni.


Pedro aliyeaminika angetua katika kambi ya Manchester United siku yoyote kutokana na yeye mwenyewe kuonyesha nia hiyo leo hii amewaacha midomo wazi viongozi na mashabiki wa timu hiyo na  wasijue kile kilichofanyika nyuma ya pazia.



Hii si mara kwanza kwa Mourinho The Specail one kama mwenyewe anavyopenda kujiita Kuwapokonya Mashetani wekundu tonge mdomoni Miaka kadhaa iliyopita pale alipoweza kumsaini kiungo kutoka Nigeria Michael Obi ikiwa tiyari kila kitu kimeshafanyika.Pedro amejiunga na Chelsea baada ya kufudhu vipimo vya afya leo hii.

HIKI NDICHO CHELSEA WALICHOKUMBANA NACHO KUTOKA KWA MAN CITY




Hatimaye ile mechi iliyokuwa ikisubiliwa kwa hamu na kupewa jina la Super Sunday imemalizika kwa Mashabiki wa Chelsea kuondoka vichwa chini baada ya kuambulia kipigo takatifu kutoka kwa Man City.


Alikuwa ni Sergio Aguero aliyefungua ukarasa wa mabao katika kipindi cha kwanza dk 32 kwa kuichambua ngome ya chelsea na kutumbukiza mpira kimiani.









vicent Kompany dakika ya 79 aliongeza bao la pili na dakika tano kabla ya filimbi ya mwisho Fernandinho alihiitimisha bao la tatu katika mchezo huo.






Katika mechi iliyochezwa awali Arsenal walifanikiwa kuibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Crystal Palace magoli ya  kifungwa na Giroud na Damien Delaney (OG ) baada ya Alex sanchez kutoa kashikashi  wakati goli la kufutia machozi la CP lilitupiwa kimiani na  Ward







JIKUMBUSHE ATLETICO BILBAO WALIVYOIADHIBU BARCA SUPER CUP

Ijumaa ya tarehe 14 Aug 2015 ilikuwa siku mbaya kwa wachezaji na masahabiki wa timu ya Barcelona pale walipochezea kichapo cha Mbwa mwizi kutoka kwa Altetico Bilbao timu hizo zilipokutana katika mchezo wa kuwania kombe la Super cup.


TIZAMA MAGOLI MATAMU YA MECHI ZILIZOCHEZWA JANA


Leo nimekuletea magoli Matamu yaliofungwa katika mechi za jana baina ya sunderland vs Norwich, Southapmton vs Everton,Tottenham vs Stokes city pamoja na  Swansea vs Newcastle. 

SUNDERLAND VS NORWICH

SOUTHAMPTON VS EVERTON

TOTTENHAM VS STOKE

SWANSEA VS NEWCASTLE



HAYA NDIO MATOKEO YA MECHI ZA LEO EPL


Ligi ya Uingereza imeendelea leo baada ya jana timu ya Manchester United kuendeleza wimbi la ushindi baada ya kuifunga AstonVilla 0-1 bao lililofungwa na mshambuliaje wake Adnan Januzaj.






Mechi za leo zilikutanisha timu 6 za ligi hiyo na matokeo mpaka mwisho wa mechi yalikuwa kama ifuatavyo.

FULL TIME SCORES

Southampton 0-3 Everton

Sunderland 1-3 Norwich

Swansea 2-0 Newcastle

Tottenham 2-2 Stoke

Watford 0-0 West Brom

West Ham 1-2 Leicester



Alikuwa ni mshambuliaji kutoka ubelgiji Romeo Lukaku aliyeiwezesha Everton kuibuka na ushindo mnono baada ya kufunga magoli mawili kipindi cha kwanza dakika ya 22 na 45 na kuiwezesha Everton kuibuka na ushindi wa goli 3 -0 , R.Barkley alihitimisha goli la tatu dakika ya 82.









Kesho Ligi hiyo inatazamiwa kuendelea pale Manchester City itakapo ikaribisha Chelsea na Crystal Palace itakapo ikaribisha Arsenal.

JIONEE MAGOLI 30 BORA LIGI KUU ULAYA

Mwana Azapound Mpenda michezo pata uhondo wa kuangalia Magoli 30 bora yaliyofunga katika ligi kuu Mbalimbali za Ulaya..



FERRARI!!!

amaizing

SOCCER BONANZA

Kwako Mwana Azapound, Azapound BONANZA ipo mbioni stay tune, Stay in touch lini na wapi jibu
litawajia hapa hapa....................




NJOO TUFURAHI NJOO TUJENGE UMOJA...MICHEZO NI FURAHAAAAA