Afya
YAJUE MATUMIZI YA BAKING SODA KWA AFYA YAKO
Katika Makala hii ntakuletea matumizi mbalimbali ya Baking soda kwa jina lingine inafahamika kama Bircabonae of soda, Matumizi makubwa ya unga huu kama ilivyozeeleka na wengi ni kwa ajili ya chakula hasa kwa unga wa ngano,lakini yapo matumizi mengi mbalimbali tofauti na hilo moja ambalo limezoeleka leo na wengi.
JINSI YA KUNG'ARISHA MENO KWA KUTUMIA BAKING SODA
1. ‘Baking’ Soda:
Chukua baking soda mara moja kwa wiki, weka kwenye mswaki wako sugua meno utaona jinsi yatakavyotoa uchafu hasa rangi nyekundu.
2. Baking Soda na chumvi
Hii pia inasaidia kwa kiasi kikubwa kung’arisha meno.
Mbali na kung’arisha, chumvi pia husaidia kuua vijidudu wanaokaa kwenye meno.
Chukua maji safi, unga kiasi wa baking soda, changanya na chumvi kisha piga mswaki.
Hakikisha humezi kabisa maji hayo kwani si mazuri kwa afya, ni kwa ajili ya kupigia mswaki tu.
Pia usitumie kila siku, tumia mara moja kwa wiki.
3. Baking soda na ‘hydrogen peroxide’:
Ukichanganya vitu hivi viwili vinasaidia kutibu wadudu wanaoshambulia meno na mdomo.
Ni nzuri zaidi kwa wale wenye tatizo la kutokwa na harufu mdomoni.
4. Maganda ya ndizi mbivu-(Banana Peels):
Chukua maganda ya ndizi mbivu sugua meno yako kwa uangalifu ili usijichubue, baada ya kusugua taratibu chukua mswaki pitisha ili kuondoa mabaki ya maganda hayo.
5. Sabuni ya kufulia nguo
Sabuni ya kawaida ya kufulia nguo ni nzuri zaidi kuliko hata dawa ya mswaki, inasaidia kutakasa meno na inaua vijidudu.
Tenga siku mbili kwa wiki, hakikisha unatumia sabuni kuosha meno yako, chunga usimeze maji yake kwani yana madhara.
Tukutane tena
0 comments: