simulizi

Mwalami Kwengwegu Mwana wa Azapound aliyebobea katika Uzalishaji Tumbaku

12:31 PM tibazetuasili 0 Comments


Jina Mwalami kwengwegu si jina geni miongoni mwa wana wa azaniaalumni2000, elimu yake ya awali aliipata katika shule ya Msingi Mburahati iliyopo wilaya ya Kindondoni. na Mwaka 1997 jina Mwalami Rashid Kwengegu lilikuwa kati ya majina 450 yalioidhinishwa na Baraza la Mitihani kwenda kujiunga na shule ya Secondary Azania. Hapo ndipo safari rasmi kuelekea Mafanikio yake ya Ujasiriamali ya hivi sasa ilipoanza.

kati ya Wanafunzi 40 waliounda darasa la Form I H Mwalami Kwengegu alikuwa ni mmoja wao, wengi waliweza kumtambua kwa haraka kutokana na jina lake Kwengwegu kuonekana kama ni moja ya dawa za asili au mojawapo ya mji mkongwe barani Afrika.aliweza Kuhitimu elimu yake hiyo akiwa darasa la Form IV M na kuwa ni miongoni mwa wana wa azapoound alieacha kumbukumbu tele shuleni hapo.

Kwasasa Mwalami Kwengwengu ni Mjasiriamali aliyejikita zaidi katika uzalishaji wa zao la Tumbaku Mkoani Tabora mwenye ufahamu wa hali ya juu kiuwekezaji katika sekta hiyo nyeti inayolipatia Taifa pato kubwa sana kutokana na malighafi hiyo kuwa chanzo kikuu kinachotegemewa katika utengenezaji wa sigara nchini.

Mwalami Kwengwegu akiwa katika moja ya ukaguzi wa mashamba yake ya tumbaku kwa ukaribu zaidi

Mwalami Rashid Kwengwegu anapenda kuwakaribisha wana wa azanialumni2000 wote kujitokeza kiushauri au kiuwekezaji katika sekta hiyo.

Mwisho
Azaniaalumni2000 inapenda kumtakia Mwalami Kwengwegu kila la kheri  katika Ujasiriamali wake huo.
 Contacts: 0714 306 600

You Might Also Like

0 comments: