jamii

HONGERA GODFREY MNZAVA KWA KUUWACHA UKAPELA

8:56 AM tibazetuasili 0 Comments



Chama cha Makapela cha Azapound wakiongozwa na Twahir Abbas,Nuhu Magwai,Francis Ambali na Mwenyekiti wa azaniaalumni2000 na wengine wengi siku ya tarehe 05 Jul 2015 katika Kanisa la SDA Sinza kilipata pigo kubwa sana kwa kuondokewa na Mwanachama wake wa muda mrefu ndugu Godfrey Mnzava, hakika pigo hilo haliwezi kusahaulika mapema.Aidha chama cha Wanandoa kikiongozwa na katibu wa azaniaalumni2000Omary Pengo,Issa Masoud,Diaz Batholomeo,Said Mselem,  na wengineo wengi  kimempa rasmi uwanachama mpya Ndugu Mnzava kwa kumuwasa mengi na mazuri yaliomo kwenye chama hicho.
Azaniaalumni inampa pongezi nyingi sana kwa kuanza maisha mapya yenye changamoto nyingi sana katika chama hicho,kila la kheri na fanaka ndugu Godfrey Mnzava na Mke  wako Loveness Mungu awajaalie maisha yenye amani na furaha tele.Amina

               
Bwana na Bibi Harusi wakitoka Kanisani  mara baada ya kula kiapo cha raha na shida,kufa na kuzika milele amina.

Bwana na Bibi Harusi wakiingia ukumbini,they look so Gorgeous!!!!!


Mapenzi raha Jamani, Bibi harusi akimnong'oneza jambo husband wake wakati wa sherehe katika ukumbi wa Hekima Garden Mikocheni

  Nilishe nikulishe ndio ishara ya upendo eheee

  cheers ndio neno pekee lifaalo hapa,Bwana na bibi harusi wakigonga cheers, kama ishara ya kuunganisha mapendo yao pamoja
 Best Woman wakiwa katika pozi na Bibi harusi Loveness katika fukwe moja bora kabisa jijini      Dar es salaam

Best Man wa Bwana Harusi katika pozi la pamoja mara baada ya harusi kuisha,fantastic

Mrs Mnzava akiwa katika pozi bora kabisa,Hongera Godfrey Mnzava kwa kupata Mke bora maishani

Mr and Mrs Mnzava wakiwa Safarinii  kuelekea Honeymoon


"Husband and Wife" wakijiandaa kupanda ndege  kuelekea  moja ya visiwa vilivyopo Tanzania kwa ajili ya kwenda  kufarahia fungate yao 


CONGRATULATIONS..............................................

You Might Also Like

0 comments: