Uchumi

AZAPOUND BANK ACCOUNT

10:25 AM tibazetuasili 0 Comments

Kuhusiana na kufungua akaunti,

Kama nilivyoahidi siku ya jumamosi kuwa jumatatu tungepata namba ya akaunti yetu, lakini haikuwa hvyo naomba radhi sana kwa hilo, na kwa bahati mbaya sana kibarua kikanibana, nikashindwa kufika pale tangu jumatatu, na pia sikuona simu kutoka kwao, ikanipa mashaka, kiasi cha kufanya jitihada kufika pale leo mchana.

Nilipofika nikapata kujua kuwa kuna sehemu ya katibu mkuu wa Azania alumni 2000 hapajasainiwa bado, na ni kutokana na wao kusema watafungua akaunti, atasaini baadae, lakini meneja wa tawi alitaka lazima pasainiwe ndio akaunti ifunguliwe, hvyo kesho, Katibu mkuu ndugu Simon Matere atafika pale kutia sahihi, na akaunti kufunguliwa.

Kuhusiana na swali la kaka Deo Katundabwile alilouliza leo asubuhi, je watu walio nje ya Tanzania watawezaje kuweka pesa kwenye akaunti ya kikundi wakiwa huko?, swala hilo litakuwa sio tatzo, wanaweza kuweka hela huko walipo, kwani TPB, imejiunga na Standard Chartered Bank na Bank of Baroda, ambazo zinatoa huduma kimataifa, na zina matawi  nchi nyingi, malekezo jinsi gani ya kufanya utayapata utakapofika benki zilizotajwa hapo juu.

Napenda kutoa pendekezo, wale walioweka pesa yao ya kuanza zoezi la kudeposit mwezi huu, basi wakae nazo tayari kwa kuanza kutunisha mfuko, maana zoezi linaanza rasmi mwezi, au niseme wiki hii.

Na kuhusiana na idadi gani ya wanachama walio hai, tuna wastani wa wanachama wasiozidi sabini na tano, hvyo tegemeeni mkono wa chuma kupita wiki hii ili kuziba hilo gape la wanachama wasio hai.

Hivyo basi kama kuna mtu ana namba za wana Azania alumni 2000 ambao wako tayari, na hawako humu, tafadhali tumeni namba zao inbox yangu ili niwa-add.

Ahsante sana,

Mwinyi Hassan

Mwenyekiti Azania alumni 2000.

You Might Also Like

0 comments: