Uchumi

PANGANI KULALA NA NJAA KUPENDA

12:17 PM tibazetuasili 1 Comments


"Pangani kulala na njaa kupenda " ndio kauli mbio yetu sote, twende Pangani, wana Azaniaalumni tunaombwa kutupia mchango wa kukuza uchumi kiasi chochote kile ulicho jaaliwa ili kutimiza adhima ya kujiinua kiuchumi ili tuweze kununua Ardhi iliyopo pangani yenye ukubwa wa ekari 33 kwa gharama ya Tsh 20M.



 Kwa mujibu wa timu iliyotembelea eneo hilo ndugu Ntimi Mwakipake, Mwinyi Hassani,  Ayubu Misheli na Allan Rwechungura eneo hilo ni HOT CAKE  lenye rutuba tele na lililo  pembezoni mwa mto Pangani ,eneo lina hati miliki zote za kiserikali na linafikika kwa njia zote za usafiri, TUPIA TPB  TWENDE PANGANI.



Eneo hilo pia limepakana na Shamba kubwa la Bepari mmoja aliyebobea kwenye kilimo cha umwagiliaji wa kisasa kitu ambacho kitaleta changamoto za kupata ujuzi kama Azaniaalumni wataamua kuwekeza kwenye kilimo, vilevile eneo linafaa kwa uwekezaji wa ufugaji wa samaki kitu ambacho Azania alumni wanajivunia kuwa na Mtaalam wa Ufugaji Afrika Mashariki ndugu Ayubu Misheli.


JE ni nani tunayemtaka aje ili atuwezeshe kulichukua eneo hilo potential kwa faida zetu kama sio sisi wenyewe wana AZAPOUND?

"TUPIA TPB TWENDE PANGANI"

You Might Also Like

1 comment:

  1. Hakuna wa kutuwezesha zaid ya sisi wenyewe kujitoa kwa michango yetu ili kufanikisha kununua shamba hilo kwa ajili ya matumizi anuwai kwa manufaa ya wana Azania Alumni 2000..Pangani Mpango Mzima

    ReplyDelete