jamii

PUMZIKA KWA AMANI AZIZ PONERA

7:41 AM tibazetuasili 0 Comments


Mwili wa aliyekuwa mwana azapound mwenzetu Aziz Ponera aliyefariki usiku wa kuamkia tarehe 09/07/15 kwa ajali ya moto nyumbani kwao umezikwa leo tarehe 10/07/15 katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam,ama kwa hakika ni majonzi makubwa kumpoteza kijana mwenzetu,Familia ya Marehemu inatoa shukrani za dhati kwa ndugu, majirani na marafiki wote walioshiriki kwa namna moja au ingine mpaka kufanikisha kumpumzisha ndugu yetu katika nyumba yake ya milele,Mungu Ilaze roho ya Marehemu Mahali pema Peponi,Amina

Katika Mazishi hayo Azaniaalumni2000 ilifanikiwa kuwakilishwa na baadhi ya wajumbe pamoja na Viongozi wa ngazi ya juu wa Jumuiya hiyo.

Wana wa Azaniaalumni2000 waliobahatika kushiriki maziko ya mwenzetu Aziz Ponera wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya maziko kukamilika


 


Mwenyekiti wa Azaniaalumni2000 ndugu Mwinyi Hassan akiomba dua katika kaburi la Marehemu mara baada ya maziko kuisha,chini katibu wa Azaniaalumni2000 akipokea dua ya kumuombea Marehemu apumzike kwa amani

               

Wana wa Azaniaalumni2000 wakitoka katika maeneo ya makaburi ya kisutu mara baada ya maziko kukamilika

Mwisho kabisa Mwenyekiti anawatakia kila la kheri kwa wale wote waliobahatika kushiriki maziko ya mwenzetu pamoja na wale waliojaaliwa kutoa rambirambi zao, Mungu awazidishie na awajaalie wale ambao hawakubahatika kujaaliwa kutoa.
AZAPOUND FOR LIFE





You Might Also Like

0 comments: