jamii
Wengi Wajitokeza Kumfariji Mfiwa
Faraja ni jambo zuri sana hasa pale unapopatwa na Masahibu, hivyo ndivyo Wana wa Azapound walivyofanya kwa mwenzao Ntimi Omega Mwakipake kwa kujitokeza kwa wingi kwenda kumpa faraja baada ya kuondokea na baba mzazi usiku wa tarehe 17 Jul 15, ama kwa hakika ni jambo zuri linalotia faraja miongoni mwa umoja huu.Mazishi ya mzee Mwakipake yanatarajiwa kufanyika kesho katika makaburi ya Kinondoni, Wana Azapound mnaombwa kujitokeza kwa wingi ili kushiriki mazishi hayo.
Ntimi Mwakipake wa tatu kutoka kulia akibadilishana maneno na baadhi ya wana wa Azapound pindi walipoenda kumpa faraja nyumbani kwao Osterbay
0 comments: