michezo

PEDRO ATUA RASMI CHELSEA BADALA YA MAN UTD

12:09 PM tibazetuasili 0 Comments


"Maisha bila fitina hayaendi" kauli wapendayo kuitumia vijana wengi wa  kisasa, kauli hiyo imedhihirika masaa machache yaliopita baada ya Club ya Chelsea  kufanikiwa kuinasa sahihi ya  mchezaji wa Barcelona Pedro Rodriguez, 28 kwa ada ya Euro M30 na kuwaacha mashabiki wa Manchester United midomo wazi wasijue sintofahamu hiyo ama unaweza kusema wamenyan'gwa tonge mdomoni.


Pedro aliyeaminika angetua katika kambi ya Manchester United siku yoyote kutokana na yeye mwenyewe kuonyesha nia hiyo leo hii amewaacha midomo wazi viongozi na mashabiki wa timu hiyo na  wasijue kile kilichofanyika nyuma ya pazia.



Hii si mara kwanza kwa Mourinho The Specail one kama mwenyewe anavyopenda kujiita Kuwapokonya Mashetani wekundu tonge mdomoni Miaka kadhaa iliyopita pale alipoweza kumsaini kiungo kutoka Nigeria Michael Obi ikiwa tiyari kila kitu kimeshafanyika.Pedro amejiunga na Chelsea baada ya kufudhu vipimo vya afya leo hii.

You Might Also Like

0 comments: