simulizi

JE ULISHAWAHI KUMSIKIA BORNIFACE CHAMADALI?

10:53 AM tibazetuasili 0 Comments

Wana wa Azapound wengi wakitajiwa jina la Borniface Chamadali na kuulizwa je wanamfahamu mtu huyo kama alishawahi kusoma Azania? basi majibu ya wengi yatakuwa Hapana jina hilo au mtu huyo hakuwahi kutokea katika kizazi cha waliobahatika kupita katika shule hiyo. 
Borniface Chamadali ndio Diaz Batholomeo Je ulikuwa ukilifahamu jina hili? la hasha kama ukiwa ni miongoni mwa uliokuwa ulkilifahamu jina hili basi ni miongoni mwa wanafunzi wachache sana kati ya wengi waliokuwa hawajui kitendawili hiki.


             

Borniface Chamadali au Diaz Batholomeo kama wengi wanavyomfahamu kwasasa ni Mwalimu wa Sekondari katika shule ya Masaki iliyopo Kisarawe akifundisha somo la kemia na Baiologia, huwezi amini katika shule hiyo Diaz amegeuga kuwa nguzo kuu na muhimili sana katika masomo hayo kutokana na style ya ufundishaji wake ambayo  imepelekea wanafunzi wengi kupenda masomo hayo.


Siri hii Mwenyewe Diaz anabainisha imetokana na kupitia mazingira mengi tofauti yaliompa ujuzi mwingi alipokuwepo Azania ( O'level ) na shule ya secondary Usagara ( A'level) ama kwa hakika azaniaalumni2000 tunapaswa kujivunia kwa kile wajumbe wake wanavyochangia michango mikubwa katika jamii kutokana na taaluma zao.



Diaz kwasasa amevishwa kofia ya ukatibu msaidizi wa azaniaalumni2000 baada ya kuchaguliwa na wajumbe wengi kutokana na taaluma yake ya uwalimu aliyonayo.


Azaniaalumni2000 inamtakiwa kila la kheri Diaz katika Taaluma yake ya kuelimisha wadogo zetu na Taifa kiujumla Mungu amzidishie maarifa mapya kila siku.




You Might Also Like

0 comments: