jamii

JE UMEPATA MREJESHO WA KIKAO CHA KUPITISHA KATIBA?.. KAMA BADO USOME HAPA

9:57 AM tibazetuasili 0 Comments

MUHTASARI WA MKUTANO MKUU WA AZANIA ALUMNI 2000 WA KUPOKEA,
KUJADILI NA KUPITISHA RASIMU YA KATIBA ULIOFANYIKA TAREHE 13/09/2015
KATIKA HOTEL YA DON SUITE- ILALA BUNGONI.

MAHUDHURIO:-
NA
JINA
CHEO
1
BW. MWINYI HASSAN
MWENYEKITI
2
BW. SAID MSELEM
M/MWENYEKITI
3
BW. DIAZ BARTHOLOMEO
M/KATIBU
4
BW. HILORIMS MAYOMBO
MJUMBE
5
BW. JOSEPH MWAISEMBA
MJUMBE
6
BW. JOSHUA CHALE
MJUMBE
7
BW. VICTOR MKAMA
MJUMBE
8
BW. FIDELIS . C. BUGOYE
MJUMBE
9
BW. FRANCIS MKUMBUKWA
MJUMBE
10
BW. JUMAA WAZIRI
MJUMBE
11
BW.ADOLF NDEGE
MJUMBE
12
BW. SAID KHAMIS
MJUMBE
13
BW. ADOLPH GERALD
MJUMBE
14
BW.MAMBYA SOSPETER
MJUMBE
15
BW. NUHU MAGWAI
MJUMBE
16
BW. COSTANTINO L. KINAWIRO
MJUMBE
17
BW. PETER  .D. NYAKACHARA
MJUMBE
18
BW. BAKARI .R. MBAGA
MJUMBE
19
BW.FRANCIS .R. AMBALI
MJUMBE
20
BW. MASOUD SHUKURU
MJUMBE
21
BW. SHEBA COSMAS SUNZU
MJUMBE
22
DR.MBONEA H. MRANGO
MJUMBE
23
BW.NEWTON MASANZU
MJUMBE
24
BW.GODFREY R. VALERIAN
MJUMBE
25
BW.MWARAMI R. KWENGWEGU
MJUMBE
26
BW.OMARI SAID
MJUMBE
27
BW. SUDI PONGWE
MJUMBE
28
BW.STEPHEN N. MTAWA
MJUMBE
29
BW.SHOLLA G. MANONI
MJUMBE
30
BW.JUMANNE S. NGAKONDA
MJUMBE
31
BW.TWAHIR KIOBYA
MJUMBE
32
BW. GODFREY NZAVA
MJUMBE
33
BW.NTIMI O. MWAKIPAKE
MJUMBE
34
BW. MOHAMED HABIBU
MJUMBE
35
BW. CHACHA WAMBURA
MJUMBE
36
BW. SALES EZRA
MJUMBE
37
BW. GODFREY GORDIAN MWESIGWA
MJUMBE



KUFUNGUA KIKAO
Mwenyekiti alifungua kikao mnamo saa 5:10 asubuhi na kutoa neno fupi kwa niaba ya Sekritarieti yote, alizungumzia changamoto zilizopo , ikiwa ni pamoja na uhudhuriaji wa vikao vya umoja huu, pia alitoa taarifa ya udhuru kwa baadhi ya wajumbe akiwemo katibu wa Azania Alumn 2000 vilevile Mwenyekiti alitoa historia fupi ya Azania Alumni 2000, ambapo alisema Azania Alumni 2000 ilihasisiwa na Bw. New ton Masunzu kama group la kusalimiana tu. Baadae watu wakaja na wazo la kusaidiana kijamii.Tulianza na kumsaidia Bw. Omary Hamadi (Ommy G) tulijitahidi vya kutosha kuhusu (Ommy G) mwisho wa siku tulibaini kwamba Bw. Omary Hamadi hakuwa tayari kupokea misaada yetu ndipo tulipoliacha suala lake kwa familia yake.

Maeneo mengine tuliyoshiriki ni katika matukio yafuatayo:-
-          Msiba wa baba yake Hilorims  Mayombo
-          Msiba wa mama yake Adolph Gerald
-          Msiba wa baba yake Ntimi Mwakipake
-          Msiba wa mtoto wa Charles Mrosso
-          Msiba wa mwana Azania mwenzetu Aziz Ponera
-          Msiba wa mama yake Omary Bakari.
-          Harusi ya Bw. Ntimi  Mwakipake na Godfrey Mnzava.

Malengo ya Umoja huu:-
-          Kuwa pamoja katika shida na raha
-          Kuongeza nguvu ya pamoja kujiongezea kipato
-          Kujikuza kiuchumi.

Changamoto:-
Wanachama ni wengi ila namna ya kuwafikia wote ni shida kidogo njia ni moja tu whatssapp group. Siku za mbele tutakuwa namna nyingine ya kuwa na uwezo wa kuwafikia wajumbe wengi zaidi.



Uanzishwaji wa website:-
Imeanzishwa website ya Azania Alumni 2000 ambayo ni www.azanialumn2000.blogspots. Com ilianzishwa na Bw. Masoud Shakur kwa kushirikiana na Bw. Allan Rwechungura.

Mwenyekiti aliomba wajumbe kutembelea zaidi ya kwenye Blog yetu ili tujitangaze zaidi na baadae ituingizie kipato. Pia alisisitiza kuweka pembeni itikadi za vyama vya siasa, udini na ukabila ili visije kutugawa katika umoja wetu.

Baada ya kusema hayo Mwenyekiti alimkaribisha Mwenyekiti wa rasimu ya Katiba Bw. Twahir Kiobya. Mwenyekiti wa maandalizi ya Rasimu ya Katiba alishukuru kwa niaba ya wajumbe wote wa rasimu ya Katiba na kuwapongeza kwa kutoa muda wao mwingi kukamilisha kazi hii nzito. Mwenyekiti wa Rasimu ya Katiba aliwakaribisha Wajumbe waliohudhuria kuanza kujadili ndipo wajumbe waliposhauri tuchambue kipengele kwa kipengele na tulifanya kama walivyoshauri Wajumbe. Wajumbe wamesema kuwepo na kurasa ya utangulizi inayoonyesha yaliyomo:-
-          Kila ibara isining’inie iwe kwenye kurasa moja na muendelezo wake.
-          Baadae kutakuwa na kanuni baada ya katiba hii kupitishwa, leo hii 13/09/2015.
-          Rasimu ya katiba yetu ilikuwa na jumla ya Ibara (42) kati ya Ibara hizo ibara (29)ishirini na tisa zimefanyiwa marekebisho na wajumbe waliohudhuria.
-          Rasimu ilipitishwa na wajumbe wote pamoja na marekebisho yake mnamo saa 2:30 usiku na kuwa katiba ya Azania Alumni 2000.

Mengineyo :-
Kutakuwa na kiingilio cha uwanachama na wajumbe walikubaliana kiwe ni Tsh. 20,000/= na kuwepo na mchango wa kila mwezi kiasi cha Tsh. 15,000/= kwa mwezi ikiwa ni Tshs. 5,000/= ni kwa ajili ya mambo ya jamii na Tshs. 10,000/=kwa ajili ya kutunisha mfuko wa Chama. Michango yote hii itaanza rasmi tarehe 30/09/2015, kutakuwa na muda wa kupokea michango hiyo ambapo ni tarehe 10 ya kila mwezi.

Fedha hizo zitakaa kwenye akaunti yetu ya Posta Benki. Uhalali wa mwanachama katika umoja huu utakuwa hai pale tu atakapotoa ada ya kiingilio tajwa na kutoa michango ya kila mwezi pamoja na mambo mengine kikatiba hii. Azania Alumni 2000 forever…!!

Muhtasari huu umesainiwa
Jina                                                      Sahihi.Jina                                           Sahihi
Bw. Simon Swai                                   Bw. Mwinyi Hassan
Katibu                                                  Mwenyekiti
Tarehe                                                 Tarehe..



You Might Also Like

0 comments: