Uchumi

BONDE LA MTO PANGANI LAVAMIWA SERIKALI YATOA ONYO KALI!!!

11:24 AM tibazetuasili 0 Comments


Kati hali inayopelekea kuhatarisha uhai wa mto Pangani kufuatia wavamizi waliojitokeza kando kando ya mto huo ambao wanaendesha shughuli za kilimo na wengine kudiriki kuchimba mabwawa makubwa kwa ajili ya ufugaji samaki kinyume na taratibu za hifadhi za mto huo, Serikali imetoa onyo kali na kuahidi kuwachukulia hatua kali wale wote watakaobainika kuendesha shughuli kinyume na hifadhi za mto Pangani, Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja Wizara ya Nishati na Madini zinavyosema.


Meneja wa Tanesco vituo vya umeme vya  Hane , Nyumba ya Mungu na Pangani Mhandisi John Skauti akizungumza kupitia kituo cha TV cha  Channel Ten amesema kina cha maji katika bwawa la Nyumba ya mungu kinazidi kupungua siku hadi siku kutokana na Mabepari hao waliojitokeza kando kando ya mto na kuitaka serikali kuchukua juhudi za haraka kupambana na Ujangiri huo mara moja hali inayopelekea kuhatarisha uzalishaji wa umeme katika kituo hicho kupungua kutoka Mega Watts 100 hadi 24 kitu kinachopelekea kuliingiza Taifa gizani bila sababu za msingi.



Afisa Msimamzi wa Bonde la Mto Pangani Bwana Vanderine Baso anayeshughulikia matumizi ya maji ya mto Pangani naye ameitaka Serikali kuwachukulia hatua kali wale wote walio kando kando ya mto huo na wenye matumzi makubwa kupita kiwango ambao wanahatarisha uhai wa Mto Pangani watafutwe na wafikishwe sehemu husika kama itabahinika wanafanya shughuli hizo kinyume na taratibu.

Ushauri kwa Viongozi na Azaniaalumni 2000 kuachana na michakato iliyokuwa inaendelea ya kununua Ardhi Pembezoni mwa Mto huo kusitishwa mara moja kwani hali halisi ya Bonde hilo imeshaanza kutia mashaka kufuatia onyo hilo kutoka mamlaka husika.

AZANIAALUMNI2000 FOREVER!!!!!!!!!!!!!!!!

You Might Also Like

0 comments: