Uchumi

KILA LA KHERI SAFARINI BAGAMOYO

10:38 PM tibazetuasili 0 Comments


TAARIFA!

Kwa niaba ya Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi na Mipango, ndugu Mwaisemba. Kamati inapenda kuwajulisha wanachama wote wa AA2K kua ile safari ya kwenda Bagamoyo kutafuta maeneo itafanyika siku ya Jpili  tarehe 15 Nov 2015. Safari hii ilichelewa kidogo kupisha maswala mazima ya uchaguzi wa nchi yetu. Uongozi wa kamati umeteua wajumbe wafuatao watakao tuwakilisha katika safari hiyo. 

1. Ndg, Joseph Mwaisemba-Mwenyekiti wa kamati.
2.Ndg, Mwinyi Hassan- Mwenyekiti AA2K 
3.Ndg, Simon Swai- Katibu mkuu AA2K 
4.Ndg, Francis Ambali - Mwenyekiti Kamati ya mambo ya Jamii.


Ndugu watajwa hapo juu tafadhari mnaombwa mtoe ushirikiano wenu wa hari na mali kuweza kufanikisha safari hiyo. Uongozi wa kamati ya uchumi na mipango unawatakia safari njema na mafanikio tele. Ieleweke kwamba mioyo macho na masikio yetu wote wana AA2K yatakua pamoja nanyi. Aidha kamati inaendelea kusisitiza kwa wadau wote kutosubiri mpaka june 2016 bali tuendelee kuchanga kidogo kidogo ili kuweza kukabiliana na fursa yoyote itayojitokeza hivi karibuni. Pia Kamati inapenda kuweka bayana na kudhihirsha kwamba hii ni mipango ya UCHUMI wa wana Azania Alumni 2000. Idadi ya waliochanga mpaka sasa ipo na wanafahamika kwa majina, kwa hiyo fursa itapo jitokeza yule aliye/ atakae changia ndiye atakae faidika nayo. Mungu ibariki Tanzania Mungu ibariki Azania alumni 2000. 

Asanteni Adolph Gerald Katibu - Kamati ya Uchumi na Mipango AA2K.

You Might Also Like

0 comments: