michezo
Alikuwa ni Steven Naismith aliyepeleka kilio cha pili mfululizo kwa mashabaki wa timu ya chelsea pale alipofunga hat trick na kuiwezesha timu yake ya Everton kuondoka na ushindi mnono wamabao 3 kwa nunge.
HIKI NDICHO KILICHOWAPATA CHELSEA NA LIVERPOOL ..NI HURUMA
Alikuwa ni Steven Naismith aliyepeleka kilio cha pili mfululizo kwa mashabaki wa timu ya chelsea pale alipofunga hat trick na kuiwezesha timu yake ya Everton kuondoka na ushindi mnono wamabao 3 kwa nunge.
Naismith alianza kupigilia Misumari hiyo ya moto kunako dakika ya 17, 22 na kumalizia Msumari wa mwisho katika dakika ya 82, hiki kinakuwa ni kipigo cha kwanza takatifu kwa chelsea kutoka kwa Everton toka msimu wa mwaka 1988-89.
Goli la kufutia machozi la The Blues lilifungwa na Nemanja Matic katika dakika ya 36 ya kipindi cha kwanza ya mchezo huo.
Katika Mchezo mwingine uliowakutanisha watani wa jadi Mashetani Wekundu Manchester United na Majogoo wa London Liverpool, Mchezo huo uliisha kwa Man U kuchomoza na ushindi mnono wa Magoli 3-1
Alikuwa ni Daley Blind aliyeanza kuandika bao la kwanza katika dakika ya 49 na kisha Andrew Herrera kuandika bao la pili kwa Mkwaju wa penati baada ya mlinzi kinda Gomez wa Liverpool kumshezea madhambi Herrera dakika ya 70.
Christian Benteke alifanikiwa kuifungia timu yake bao la kufutia machozi kwa tik tak kali iliyomuacha mlinda mlango David de Gea asijue la kufanya.
Alikuwa ni Anthony Martial dakika ya 86 alipowanyonyoa manyoa yote Majogoo ya London baada ya kupigilia msumari wa moto na mwisho na kuifanya Man U kuibuka kidedea kwa Jumla ya Magoli 3 -1
0 comments: