jamii
NIMEKULETEA RASIMU YA KATIBA PENDEKEZWA YA AZANIA ALUMNI 2000
KATIBA YA CHAMA CHA AZANIA
ALUMNI 2000
SEHEMU
YA I: UTANGULIZI
IBARA
1: Utangulizi:
Kwakuwa:
Maendeleo ya watu
katika jumuiya au Taifa lolote hutegemea ufahamu wa namna bora ya kutumia
rasilimali zilizopo;
Na kwa kuwa:
Umoja wa watu hao
na ushirikiano kati yao kwa njia ya kufahamiana, kusaidiana ni muhimu kwa
ujenzi wa ufahamu huo;Jukumu la kuleta maendeleo ya wanajamii wa AZANIA ALUMNI
2000 ni la wanajamii wenyewe kwa njia ya kuunganisha nguvu, juhudi na maarifa
yao na jamii na mamlaka nyinginezo;
Na kwa kuwa:
Wameunganishwa na
Umoja wao wa AZANIA ALUMNI 2000 wanachama wana jukumu la kusaidiana na
kushirikiana.
Kwa hiyo basi:
Kwa pamoja
tunaungana na kukubaliana yafuatayo:
SEHEMU
YA II: DIRA, DHAMIRA NA MADHUMUNI
IBARA
2: Dira
Kuwa Chama bora kinachohamasisha
Umoja na uelewano na chenye uwezo wa kuwawezesha wanachama wake na jamii
inayokizunguka kiuchumi na kijamii
IBARA
3: Dhamira
Kuchangia na kuleta
ushirikiano wa kijamii ili kuinua kiwango cha maisha ya wanachama kwa
kuwezeshana kama wadau ndani na nje ya Chama
IBARA
4: Madhumuni Ya Kuanzisha Chama
(i)
Kushirikiana
katika taabu na raha kama vile Sherehe, Ugonjwa na Misiba
(ii)
Kukuza
uwezo wa Chama kwa kuanzisha shughuli za
kimaendeleo na biashara
(iii)
Kushirikiana na serikali na taasisi nyingine
ndani na nje ya nchi zitakazofaa kutimiza malengo ya Chama chetu na kupokea
toka serikalini haki na misaada mbalimbali ikiwemo kuomba, kununua au kukodi
majengo au ardhi ya kufanyia kazi na rasilimali nyinginezo muhimu
(iv)
Kusaidia
vikundi vya kijamii vyenye uhitaji maalum.
(v)
Kuhamasisha
na kuwezesha shughuli za michezo kwa wanachama
SEHEMU
YA III: KATIBA, USAJILI NA ENEO LA UTENDAJI KAZI
IBARA
5: Matumizi ya Katiba
Katiba hii itatumika kwa
malengo yaliyokubaliwa na wanachama wake na kuongozwa kwa kanuni zake.
Katiba hii itaanza kutumika
mara baada ya kupitishwa na wanachama kwa asilimia zaidi ya hamsini.
IBARA
6: Jina La Chama
(i)
Jina
la chama litakuwa AZANIA ALUMN 2000
(ii)
Na
kifupi chake kitakuwa (AA2000)
IBARA
7: Usajili
Chama kitasajiliwa kwenye
mamlaka husika mara itakapoamuliwa na mkutano mkuu wa wanachama
IBARA
8: Ofisi Kuu
Makao makuu ya Chama yatakuwa
Dar es Salaam.
IBARA
9: Eneo La Utendaji Kazi
Chama kitafanya kazi Tanzania
na nje ya mipaka yake
SEHEMU
YA IV: UANACHAMA NA AINA ZA WANACHAMA
IBARA
10: Sifa za Mwanachama
(i) Awe mwanafunzi aliyemaliza
masomo ya sekondari yaani Ordinary Level mwaka 2000 katika shule ya sekondari
Azania.
(ii)
Awe
na akili timamu na mwenye kutimiza majukumu yake ya kufanya kazi za Chama.
(iii)
Awe
ameingia kwenye chama kwa hiari yake mwenyewe bila kushurutishwa na mtu yeyote
yule.
(iv) Awe analipa ada na michango
ya Chama kama itakavyopendekezwa na Chama.
(v)
Mwana
Azania 2000 atakayeomba kujiunga baada ya Chama kuanzishwa, ada yake ya
kiingilio itategemea na kiwango kitakachopitishwa na mkutano mkuu, sambamba na
maombi yake kujadiliwa na mkutano huo.
IBARA
YA 11: Haki za Mwanachama
a. Kupata taarifa za shughuli za
Chama kwa kufuata taratibu
b. Kuchangia mawazo, fikra na
maoni mbalimbali katika Chama
c. Kuchagua au kuchaguliwa
kushika nafasi mbali mbali za uongozi
d. Kufanya kazi za Chama kama
zinavyomhusu
e. Kuhudhuria vikao na
mikutano ya Chama inayomhusu
f.
Kuwa
tayari kupambana na aina yoyote ya uonevu, ukandamizaji udhalilishaji na
ubaguzi ndani ya Chama kwa kuzingatia sheria za nchi
g. Kujitetea, kusikilizwa,
kuheshimiwa na kukata rufaa anaposhitakiwa ama kuchukuliwa hatua za kinidhamu
ndani ya Chama
h. Kila Mwanachama anayo haki ya
kuchangiwa kwenye msiba, sherehe, magonjwa au tatizo lolote ambalo kamati ya
jamii na sekretarieti ya chama itaona umuhimu wake.
i.
Mwanachama
anayo haki ya kujitoa na stahiki zake atazipata kutegemeana na kanuni zilizopo
na sababu zake za kujitoa. Mwanachama atakayejitoa au kufukuzwa kwenye chama
atakuwa amepoteza stahiki zake zote.
j.
Mwanachama
atataja jina la Mrithi wake na anaweza kubadili jina la Mrithi wake wakati
wowote, Mrithi atakuwa na haki zote za marehemu isipokuwa haki ya uanachama
k. Mwanachama ana haki ya kupata
haki sawa na wanachama wengine
IBARA
YA 12: Ukomo wa Uanachama
(i)
Kutokana
na mwenendo usioendana na madhumuni , kanuni za maadili na sera za chama
(ii)
Kujitoa AZANIA alumni
kwa hiari yake mwenyewe
(iii)
Kutolipa
ada na michango ya chama kwamuda wamiezi mitano mfulilizo
(iv)
Kuugua
ugonjwa wa akili baada ya kuthibitishwa na daktari utakaopelekea kushindwa
kutimiza wajibu wake wa uanachama.
(v)
Kushindwa
kuhudhuria mikutano ya chama au vikao bila ya sababu ya kuridhisha kwa kipindi
cha miezi kumi na miwili mfululizo
(vi)
Mwanachama
akishindwa kuhudhuria mikutano mikuu mitatu mfululizo bila taarifa rasmi
IBARA
YA 13: Wajibu wa Mwanachama.
(i)
Kujadili
na kupitisha mipango ya shughuli zinazohusu chama
(ii)
Kujadili,
kuthibitisha na kupitisha mapato na matumizi ya chama
(iii)
Kujadili
nidhamu ya wanachama na katika kupendekeza hatua za kuchukua
(iv)
Kufanya
shughuli za chama kama inavyompasa.
(v)
Kuchangia
gharama za uendeshaji chama kwanjia za ada na michango iliyoamuliwa na chama
(vi)
Kuwa
tayari kupambana na aina yeyote ya uonevu, ukandamizaji, udhalilishaji na
ubaguzi ndani ya chama kwa kuzingatia sheria za nchi.
(vii)
Hakuna
mwanachama mwenye nafasi yakuridhia au kutoa wazo la kuvunjika kwa umoja huu.
(viii)
Kulinda
na kutetea katiba halali ya Azania Alumni 2000 iliyopitishwa na wanachama
katika mkutano mkuu.
SEHEMU YA V SIFA NA MUUNDO WA UONGOZI
IBARA
YA 14: Sifa za Uongozi
(i)
Awe
mwanachama aliyelipa michango ya chama kwa muda wamiezi mitatu(3) mfululizo
(ii)
Asiwe
mwenyekiti au kiongozi wa chama chochote ambacho kitaathiri shughuli za chama.
(iii)
Awe
anajua kusoma na kuandika lugha ya Kiswahili
(iv)
Awe
mwanachama kwa muda wamiezi 12
(v)
Awe
na upeo wa kuchambua, kujadili masuala ya chama na maendeleo yake
(vi)
Awe
mwaminifu, mwenye moyo wa kujitolea nakupenda kupokea ushauri kwa wenzake
(vii)
Kiongozi
anatakiwa mwenye afya njema ya kumuwezesha kusoma, kuandika na kusimamia
shughuliza chama
(viii)
Awe
mwaminifu, mwenye kujitolea na kupokea mawazo ya wenzake
(ix)
Asiwe
amewahi kufukuzwa uanachama kwa makosa ya hujuma, ubadhirifu, wizi na mali ya
chama.
IBARA
YA 15: Sekratariat
Kutakuwa na chombo cha juu
cha uongozi kitakachojulikana kama Sekratariat kitakachoundwa na viongozi
wafuatao
(i)
Mwenyekiti
(ii)
Makamu Mwenyekiti
(iii)
Katibu
(iv)
Naibu Katibu
(v)
Mweka
Hazina
IBARA
YA 16: Mweyekiti
Kutakuwa
na mwenyekiti atakayechaguliwa kwa wingi wa kura katika mkutano mkuu wa chama
IBARA
YA 17: Majukumu ya Mwenyekiti
(i)
Mwenyekiti
ndio kiongozi mkuu wa chama
(ii)
Mwenyekiti
wa mikutano mikuu ya chama isipokuwa mikutano ya kamati.
(iii)
Kuitisha
mikutano kwa kuzingatia katiba na kalenda ya chama kwa kusaidiwa na Katibu Mkuu
(iv)
Kuitisha
mikutano ya dharura
(v)
Mlinzi
na msimamizi mkuu wa katiba
(vi)
Atasaini
mikataba yote iliyoridhiwa na chama
(vii)
Msemaji
mkuu washughuli na maamuzi mbalimbali ya chama.
(viii)
Msimamizi
na mfuatiliaji wa utekelezaji maazimio ya chama
YA
18: Makamu Mwenyekiti
Kutakuwa na makamu mwenyekiti atakayepigiwa kura
kwa nafasi ya mgombea mwenza.
YA
19: Majukumu ya Makamu Mwenyekiti
Kukaimu
shughuli za mikutano kwa niaba ya mwenyekiti wakati mwenyekiti hayupo.
IBARA
YA 20: Katibu Mkuu
(i)
Mratibu
na mtendaji mkuu wa shughuli za chama ikiwemo kuandaa mipango mbalimbali ya
maendeleo ya chama
(ii)
Kuandaa
na kutunza taarifa mbalimbali za shughuli za chama
(iii)
Kutakuwa
na katibu mkuu wachama atakayepatikana kwa kupigiwa kura kwenye uchaguzi mkuu wachama
IBARA
YA 21: Naibu Katibu Mkuu
Kutakuwa na Naibu Katibu Mkuu
ambaye kazi yake itakuwa ni kukaimu shughuli za Katibu Mkuu
IBARA YA 22:
Mweka Hazina
Kutakuwa
na mweka hazina mwenye taaluma ya uhasibu ambaye shughuli zale zitakuwa kama
ifuatavyo
1.
Kutunza
kumbukumbu zote za fedha za Chama
2.
Kuhakikisha
kuwa fedgha za chama zinatolewa kwa kuzingatia taratibu za fedha na katiba
3.
Msimamizi
mkuu wa ukusanyaji wa michango, ada na mapato mengineyo ya chama kwa kufuata
taratibu za chama.
4.
Kuandaa
na kutoa taarifa za mapato na matumizi ya chama kwenye vikao vya chama,Mkutano
Mkuu na pale zitakapohitajika.
IBARA YA 23:
Ukomo wa Uongozi
1.
Viongozi
wote wa Sekratariat watadumu madarakani kwa muda wa miaka miwili baada ya
kuchaguliwa na wanaweza kugombea tena kuchaguliwa kwa vipindi vingine baada ya
hapo.
2.
Viongozi
wote wa Sekratariat watachaguliwa na mkutano mkuu wa chama kwa wingi wa kura.
3.
Uongozi
uliopo madarakani utatakiwa kukabidhi madaraka na ofisi za chama wiki mbili
baada ya uongozi mpya kuchaguliwa
4.
Madaraka
ya kiongozi yeyote yatakoma iwapo kiongozi huyo atapoteza sifa za uongozi kwa
mujibu wa ibara ya 14.
5.
Kujiuzulu
6.
Kuondolewa
7.
Kifo
8.
Kushindwa
kutimiza majukumu yake kikatiba
9.
Kufutwa
uanachama
IBARA YA 24: Kiongozi Kuondoka Kabla ya Muda
Wake
(i)
Ikiwa
mwenyekiti au katibu ataachia madaraka
kabla ya muda wa uchaguzi, makamu wake atashilikia nafasi hiyo moja kwa moja.
Sekretarieti itamteua mwanachama yeyote anayefaa kushika nafasi ya makamu ambae
atathibitishwa na mkutano wa wanachama unaofuata kwa wingi wa kura. Ikiwa
wanachama hawataridhika na uteuzi huo, wanachama watapendekeza majina matatu
kisha kupigiwa kura. Mshindi atapatikana kwa kupata kura nyingi.
(ii)
Bila
ya kuathiri Ibara ya 20 , Ikiwa mweka hazina ataachia madaraka kabla ya muda wa
Uchaguzi basi Sekratariat itamteua mwanachama yeyote anayefaa kushika nafasi
nafasi inayofuata na atathibitishwa na mkutano wa wanachama unaofuata kwa wingi
wa kura. . Ikiwa wanachama hawataridhika na uteuzi huo, wanachama watapendekeza
majina matatu kisha kupigiwa kura. Mshindi atapatikana kwa kupata kura nyingi.
IBARA YA 25:
KUKASIMU MADARAKA
Iwapo
Mwenyekiti hayupo, majukumu yake yatachukuliwa na Makamu Mwenyekiti, Iwapo
Makamu Mwenyekiti hayupo madaraka yatachukuliwa na Katibu, Iwapo Katibu hayupo
Madaraka yatachukuliwa na Naibu Katibu.
SEHEMU YA VI:
MIKUTANO
IBARA
26: Mkutano Mkuu wa Mwaka
Kutakuwa na mkutano mkuu wa
mwaka wa wanachama wote utakaofanyika kulingana na kalenda ya chama ili
kupitisha maazimio na mambo mengineyo kama yalivyoelezwa katika katiba hii kwa
mwaka husika
IBARA
27: Mkutano Mkuu wa dharura
(i)
Kutakuwa
na mkutano maalum wa dharura kulingana na ulazima wa kufanya hivyo , na
wanachama wote wanapaswa kuhudhuria.
(ii)
Mwenyekiti
kwa kushirikiana na Sekratariati anaweza kuitisha mkutano mkuu wa dharura kama
kuna ulazima wa kufanya hivyo wakati wowote
(iii)
Mwanachama
anaweza kuomba kuitishwa kwa mkutano mkuu wa dharura kujadili jambo lolote
linalohusu chama iwapo atapata uungwaji mkono wa asilimia hamsini za wanachama
wote kwa majina yao na saini zao, Mwenyekiti atalazimika kuitisha Mkutano huo
wa dharura ndani ya muda wa siku 14 baada ya madai hayo kuwasilishwa kwa katibu
wa sekratariati na nakala kuwasilishwa kwa kamati ya maadili na mashauriano.
IBARA
28: Mikutano ya Kawaida
Kutakuwa na mikutano ya
kawaida itakayofanyika kila baada ya miezi minne ya mwaka kwa vipindi vitatu
kwa wanachama wote kujadili utekelezaji wa maazimio yaliyowekwa kwenye mkutano
mkuu na masuala mengineyo ya chama.
IBARA
YA 29: Wajumbe wa Mkutano Mkuu
i.
Wajumbe
wa mkutano mkuu watakuwa wanachama wote waliotimiza masharti yote kwa mujibu wa Ibara ya 13 ya sifa za
mwanachama
ii.
Ili
mkutano mkuu uwe halali, ni sharti uhudhuriwe angalau kuanzia theluthi ya
wanachama wote
IBARA
YA 30: Wajibu, Mamlaka, na Kazi za Mkutano Mkuu
i.
Kujadili
na kupitisha mipango ya shughuli za mwaka za Chama.
ii.
Kujadili,
Kuthibitisha na kupitisha mapato na matumizi ya Chama ya mwaka unaofuata
iii.
Kupokea,
kujadili na kutolea mmaumuzi taarifa mbalimbali zinazowasilishwa na kamati
mbalimbali za Chama
iv.
Kurekebisha
katiba.
v.
Kupokea
taarifa mbalimbali za kamati
vi.
Kuchagua
viongozi wa kusimamia chama katika nafasi zilizowekwa kwa mujibu wa katiba hii
na zile zitakazotokana na shughuli za chama kuongezeka
vii.
Kupokea,
kujadili na kutolea maamuzi ada ya kila mwezi ya kila mwanachama baada ya
kupokea mapendekezo kutoka kwa wanachama
IBARA
31: Kukasimu Madaraka ya Mkutano Mkuu
Nafasi ya Mwenyekiti na
katibu inaweza kukasimiwa kwa mwanachama yeyote atakaechaguliwa na wanachama
ili kuendesha mkutano mkuu iwapo kutakuwa na haja ya kufanya hivyo.
SEHEMU
YA VII: VYANZO VYA FEDHA, UTUNZAJI NA MATUMIZI YAKE
IBARA
32: Vyanzo vya Fedha
i.
Viingilio,
ada na michango ya hiari ya wanachama
ii.
Fedha
kutoka taasisi zinazokopesha kama itakavyoidhinishwa na wanachama
iii.
Michango
ya hiari ya wahisani, wadau wa maendeleo ndani na nje ya nchi
iv.
Michango
ya hiari toka kwa mashirika na watu binafsi
v.
Harambee
halali
vi.
Miradi
mbalimbali ya Chama
vii.
Tozo
kutokana na adhabu mbalimbali
IBARA
33: Mwaka wa Fedha na Matumizi ya
Fedha za Chama
Kutakuwa na mwaka wa fedha wa
Chama utakaokuwa unaanza mwezi Januari na kuishia Desemba.
IBARA
34: Matumizi ya Fedha za Chama
i.
Kuendesha
miradi mbalimbali ya maendeleo ili kuinua kipato cha chama na wanachama .
ii.
Kulipia
gharama mbalimbali za uendeshaji wa
shughuli za chama .
iii.
Kusaidia
jami hitaji kama itakavyopendekezwa na kuamuliwa na chama
iv.
Kusaidia
wananchama katika misiba , sherehe, ugonjwa au tatizo lolote ambalo chama
kitaridhia.
IBARA
35: Uendeshaji wa Akaunti za Benki
Chama kitakuwa na akaunti
katika benki zinazotambulika kisheria
i.
Kutakuwa
na watia saini wanne katika akaunti hizo, ambao wamewekwa katika makundi
wawili:
KUNDI A.
1.
Mwenyekiti
2.
Mweka
Hazina
KUNDI B.
3.
Mwenyekiti
au Katibu wa Kamati ya Uchumi
4.
Mjumbe
Mmoja atakayeteuliwa katika Mkutano Mkuu
ii.
Ili
kuruhusu fedha kutoka katika akaunti hizo kutumika kwa mujibu wa matumizi
yaliyoainishwa kwa mujibu wa katiba hii sharti saini mbili za kati ya watia
saini hao wanne waliodhinishwa ziwepo na
ya mwenyekiti ikiwa ni ya lazima.
IBARA
36: Taarifa za Fedha
i.
Taarifa
ya fedha itakuwa inatolewa kwa wanachama wote kwenye mikutano yote ya kila
baada ya miezi mine, Mkutano Mkuu na pale itakapohitajika.
ii.
Taarifa
itayarishwe na kuwafikia wanachama wiki moja kabla ya mkutano husika ili
kufanya uchambuzi na kujitayarisha na mkutano.
iii.
Taarifa
ya fedha ya mwisho wa mwaka inatakiwa iwe imekaguliwa na mkaguzi wa mahesabu
kutoka nje ya chama ( external auditor)
IBARA
37: Ukaguzi
wa Fedha
i.
Ukaguzi
wa mapato na matumizi ya fedha za chama utafanyika mara moja kwa mwaka
ii.
Ukaguzi
maalumu wa mapato na matumizi ya fedha za chama utafanyika wakati wowote pale
utakapohitajika
iii.
Uongozi
utawasilisha ripoti ya ukaguzi ya mapato na matumizi ya chama kwa wanachama
kwenye mkutano mkuu
SEHEMU
YA VIII: MABADILIKO YA KATIBA NA
LAKIRI
IBARA
38: Mabadiliko ya Katiba
Katiba hii inaweza
kubadilishwa na mkutano mkuu wa wanachama wa mwaka au mkutano mkuu maalum.
Marekebisho yanaweza kuletwa na mwanachama na kuungwa mkono na kupigiwa kura na
wanachama kwa wingi wa theluthi mbili au zaidi.
IBARA
39: Mhuri au Lakiri ya Chama
Chama kitakuwa na Muhuri au
lakiri yenye jina la Azania Alumni 2000. Mhuri au Lakiri ya Chama haitatumika
popote isipokuwa kwa idhini na mamlaka ya Mwenyekiti na Katibu mkuu au kiongozi
anayekaimu nafasi hizo.
SEHEMU YA IX:
KAMATI ZA CHAMA
IBARA YA 40:
Kutakuwa na kamati za chama zifuatazo
1.
Uchumi
na Mipango
2.
Mambo
ya jamii
3.
Maadili
na mashauriano
4.
Rufaa
Wajumbe wa kamati hizi idadi yao haitapungua
watu wanane
IBARA YA 41:
MAJUKUMU YA KAMATI
1. Kamati
ya mipango na Uchumi
i.
Kutafiti,
kupembua miradi mbalimbali ya chama.
ii.
kuanzisha
na kusimamia miradi ya chama kwa ridhaa ya wanachama.
iii.
Kutoa
taarifa za miradi kwa Uongozi na wanachama pale itakapohitajika
iv.
Kuhakiki
na kutunza taarifa za miradi ya chama
v.
Kushauri
chama kuhusu miradi mbalimbali
2. Kamati
ya maadili, mahusiano na mashauriano
i.
Kupokea,
kusikilza na kutolea maamuzi migogoro yote inayoathiri utendaji wa chama
ii.
Migogoro
binafsi pia inaweza kutatuliwa na kamati hii
iii.
Kuchunguza
na kupendekeza hatua za kuchukua dhidi ya kiongozi yeyote na mwanachama kwa makosa
mbalimbali yanayo athiri au yatakayo athiri heshima, taswira na utendaji wa
chama.
3. Kamati
ya jamii
i.
Kuratibu
na kushughulikia masuala yote ya kijamii kama misiba, sherehe na matukio
mbalimbali ya wanachama
ii.
Kuratibu
matukio yote yenye lengo la kujenga na kuimarisha urafiki, mshikamano na undugu
baina ya wanachama.
iii.
Kutoa
taarifa na kushiriki kikamilifu kwenye shughuli mbalimbali za chama
iv.
Kutoa
ushauri kwa sekretarieti na wanachama kuhusu masuala ya jamii
v.
Kamati
ya maadili, mahusiano na mashauriano itaweza kumuita mtu yeyote ndani ya chama
kutoa ushahidi, maelezo au taarifa zozote zitakazosaidia utendaji wa kamati.
vi.
Iwapo
migogoro binafsi isiyohusu Chama baina ya wanachama kwa ridhaa zao itatolewa
maamuzi na kamati hii, Iwapo yeyote
katika wale wenye Mgogoro hawataridhika na hukumu yake, basi hawana nafasi ya
kukata rufaa katika kamati ya rufaa.
4. Kamati
ya rufaa
(i)
Kupitia
na kutolea maamuzi rufaa zote za masuala yanayohusu Chama.
(ii)
Kamati
ya rufaa itaweza kumuita mtu yeyote ndani ya chama kutoa ushahidi, maelezo au
taarifa zozote zitakazosaidia utendaji wa kamati.
IBARA YA 42: Wajumbe wa Kamati za Chama
(i)
Kamati
ya Rufaa itaundwa na Wajumbe huru watakaotoka miongoni mwa Wanachama wote
(ii)
Kamati
ya Maadili na Mashauriano itaundwa na Mkutano Mkuu kutoka miongoni mwa Wajumbe
wa Mkutano Mkuu ambao siyo viongozi na wala wajumbe katika kamati nyingine
yoyote katika chama..
(iii)
Wajumbe
wa Kamati za Mipango na Mambo ya Jamii watateuliwa na Mwenyekiti kwa
kushauriana na Wajumbe wengine wa sekreterieti.
0 comments: