TANZIA

Familia ya Azaniaalumni2000  imepata pigo kubwa sana kwa kuondokewa na mwanafamilia wake ELIA FUNGO alie fariki alfajiri ya leo tarehe 22/08/16 katika hospitali ya muhimbili aliko kuwa amelazwa baada ya kupata ajali ya gari tarehe 19/08/2016. Bwana Ametoa na bwana ametwaa jina lake lihidimiwe. Taratibu za mazishi zinaendelea nyumbani kwao Kimara alipokuwa akiishi.



Marehemu Bwana Elia Fungo enzi za uhai wake.
  

LIJUE STAFELI TUNDA LENYE UWEZO WA KUPAMBANA NA SARATANI



Stafeli ama topetope ni tunda  linalopatikana katika mikoa ya Morogoro, Iringa Tanga, Mbeya, na baadhi ya maeneo katika jiji la Dar es Salaam. 


Tunda hili linaelezwa kuwa na uwezo wa kutibu magonjwa mbalimbali ikiwamo saratani, unaweza kulila tunda hili kama lilivyo au kutengeneza juice yake vyote uleta matokeo chanya.



USHAHIDI WA KIMAABARA

Kwa mujibu wa Jarida la Kemia na madawa la nchini Marekani la mwaka 2010 linaeleza kuwa tunda hili la Stafeli au Mtopetope kuwa lina uwezo wa kuangamiza chembe hai zenye saratani pasipo kuleta madhara katika mwili. 



Taasisi ya utafiti wa Saratani ya Nchini Uingereza (NIR) ilifanya utafiti wa kwanza kuhusu maajabu ya stafeli mwaka 1976 na kubaini kuwa majani, mizizi na tunda la stafeli, vyote vina uwezo wa kutibu saratani. 




Ingawa suala la Stafeli peke yake kutibu saratani lina mjadala lakini kutokana na majaribio zaidi ya 20 yaliofanywa yamebaini stafeli lina virutubisho vyenye uwezo wa kupambana na kupunguza makali ya saratani. Pia majaribio hayo yamebaini stafeli huua chembechembe za saratani aina 12 (cancerous cell ) ikiwemo saratani ya Matiti, Mapafu, kongosho, kibofu na tumbo.


kansa ya titi

 kansa ya Pafu

  
Kansa ya Tumbo
Stafeli lina mchanganyiko wa virutubisho wenye uwezo mkubwa wa kuthibiti  ukuwaji wa seli  za saratan mara 10,000 zaidi ya dawa ya adriamycin ambayo ndio hutumika kutibu saratani. 

              
mchanganyiko wa virutubisho vya Annonaceous na Acetogenins vilivyomo kwenye stafeli huua seli zilizoathirika na saratani tu tofauti na dawa za kisasa ambazo huua seli zilizoathirika na zisizoathirika.
Stafeli uthibiti ukuwaji wa seli za saratani bila kusababisha madhara mengine tofauti na ilivyo kwa dawa za kisasa ambazo uleta madhara kiafya kwa mgonjwa pindi atumiapo iwe zile za mionzi, sindano au vidonge.
Mwana Azaniaalumni2000 pendelea kula tunda hili mara kwa mara ili kujikinga na kunyemelewa kwa ugonjwa huu ambao umekuwa hatari dunia kwasasa.
 

♣♣♣♣♣♣♦♦♦♦♦♦♦♥♥♥♥♥ ©copyright masoud shakur

ZIJUE FAIDA ZA ULAJI WA LIMAO

Limao ni tunda lenye asili ya uchachu wengi upenda kulitumia tunda hili katika kuleta hamu ya chakula kama chachandu, lakini JE UNAFAHAMU FAIDA ZAIDI YA TUNDA HILI?


ZIFUATAZO NI FAIDA ZA ULAJI WA TUNDA HILI KAMA LIKIWA KWA USAHIHI

Kusafisha mwili

Limao husaidia kusafisha uchafu usiohitajika mwilini kwa kusaidia mmeng’enyo wa chakula na kulifanya ini kufanya kazi vizuri.

Kuweka harufu nzuri kinywani

Asidi iliyopo kwenye maji ya limao huua bakteria walioko mdomoni wanaosababisha harufu mbaya ya kinywa. Ni vizuri kama ukinywa limao baada ya kupiga mswaki ili kupata matokeo mazuri zaidi.

Kuleta nguvu mwilini

Limao baada ya kuingia kwenye mfumo wa chakula, huupa mwili nguvu. Hii husaidia kuondoa uchovu na msongo wa mawazo, sonono (depression), na wasiwasi.

Kupunguza uzito

Nyuzinyuzi za pectin (Pectin fiber) zilizomo kwenye limao husaidia kuzuia njaa na hivyo kutopata hamu ya kula mara kwa mara.

Kuongeza kinga ya mwili

Malimao yana acid, ni chanzo kizuri cha vitamin C, ambayo ni nzuri kuzuia baridi na homa. Malimao pia husaidia kuimarisha ubongo na mishipa ya fahamu kutokana na kuwa na madini ya Potassium. Vilevile Potassium husaidia kuzuia shinikizo la damu.

Kuzuia uvimbe

Cha kushangaza kabisa, ukiwa unakunywa maji ya limao mara kwa mara, unapunguza kiwango cha acid mwilini mwako. Hii ni kutokana na ukweli kuwa limao haitengenezi acid mwilini baada ya kumeng’enywa. Kutokana na hii, husaidia sana kupunguza asidi ya uric ambayo ni chanzo kikuu cha uvimbe mwilini.

Kuondoa mikunjo na makovu mwilini

Maji ya limao huweza kuondoka makovu na mikunjo kwenye ngozi. Huweza vilevile kupunguza makovu makubwa kama ukinyunyizia kila mara. Kutokana na uwezo wake wa kusafisha damu, maji ya limao huacha ngozi  ikiwa inang’aa na yenye afya.

Husaidia kukufanya uache kunywa kahawa

Je wewe ni mlevi wa kahawa na unataka njia ya kuacha ? Basi kunywa kikombe cha maji ya moto chenye mchanganyiko wa limao. Hii ni dawa tosha. Huwezi kuamini hadi ujaribu, na ukishajaribu hutoweza kurudi tena kwenye kahawa.

Je unatakiwa kutumia limao kwa kiwango gani?

Kama una uzito mdogo, chini ya kilo 70, unaweza kula nusu limao, kama umezidi kilo 70 unatakiwa kula limao zima kwa siku. Ukifanya hivi kila siku utaanza kuona mabadiliko muda si mrefu.
Karibu kwenye ulimwengu wa afya. Jaribu kutumia limao na uone uzuri na faida zake kwenye mwili wako. Jua kuwa vitu vizuri mara zote huwa havina gharama, ni vilevile tunavyoviona kila siku, cha msingi ni jinsi ya kuvitumia. Ukifanya matumizi sahihi ya vitu, hakika utaona maisha yanavyokuwa mazuri. 


Wana Azaniaalumni2000 tuanze sasa kulitumia tunda hili sisi na familia zetu!!!



BONANZA LA WATANI WA JADI SIMBA NA YANGA LANUKIA


Hayawi hayawi sasa yamekuwa ule mpambano wa soka kati ya mashabiki wa Simba na Yanga kutoka Azapound Family umeiva, baada ya tambo zinazoendelea kuzidi na kupelekea ubishi huo kwenda kuamulia uwanjani. Mashabiki hao wa timu mbili wamemuomba Mwenyekiti wa AzaniaAlumni Ndugu Mwinyi Hassani kuandaa mpambano huo kabla ya mwezi mtukufu wa Ramadhani ili kumaliza ubishi huo.




Mpaka sasa tayari wameshajitokeza baadhi ya member wakithibitisha ushiriki wao katika mtanange huo, Diaz Batholomeo yeye amesema yeye atawakilisha upande wa Yanga kama Golikipa na Omar yeye amesema yupo neutral ni mchezaji huru upande wowote ukimuhitaji atauchezea.

Kwa upande wa wanazi wa Yanga wakiongozwa na Katibu wa Azananiaalumni2000 ndugu Simoni Matere wamemwambia Diaz licha ya kuonyesha mapenzi yake kwa Mabingwa hao wa Bara msimu huu hawatakuwa tayari kumruhusu kukaa golini kwani imeonekana ni mamluki wa Simba anayetaka kuipa ushindi timu yake kijanja, na kumtaka akae mbali kabisa na kama ikiwezekana aende kuungana na mashabiki wenzie kuomboleza msiba wa timu yake, kwa kukosa ubingwa na kuendelea kubakia kushiriki makombe ya Mbuzi ( Mchangani ).

Ama kwa hakika terehe hiyo inasubiliwa kwa hamu kubwa sana ili kuona ni nani atakaye ibuka mshindi siku hiyo.

HATIMAE GAMBA LA NYOKA KUJIVUA MAGAMBA


"Hakuna Mgumu kwenye mapenzi"na hakuna awezaye kushinda na Asili ( Nature) Men are born to marry an women to be married" Mwenyekiti wa Katiba wa Azaniaalumni2000 Twahil Abbas ama almaharufu GAMBA LA NYOKA hatimae amekubali yaishe kwa kuamua kujivua magamba na kuliacha kundi la makapera likipata pigo kubwa lisilo mfano kwa kufunga ndoa na mchumba wake kipenzi.

Kwa habari zilizo rasmi na zisizo na chembe hata kidogo ya chumvi kutoka chanzo cha kuaminika cha Mwenyekiti huyo wa rasimu ya katiba na pia yeye Mwenyewe ndoa hiyo inatarajiwa kufungwa visiwani Zanzibar Mwishoni mwa mwezi wa 5/16 na kufuatiwa na sherehe kubwa katika sehemu maalumu iliyoandaliwa PORT VIEW Hotel yenye maanzali mwanana ukanda wa juu kusini mwa Zanzibar .

Ukiwa Mtu wa karibu wa Twahil Abbas unaombwa kushiriki kwa hali na mali ili kufanikisha shughuli hii, maelezo ya ufanikishaji wa shughuli hiyo tazama maelezo katika kivuli cha kadi. 
Familia ya Azaniaalumni2000 inamtakia kila la kheri Ndugu Twahil Abbas ama Gamba la Nyoka katika tukio hilo muhimu maishani.

KUTANA NA KIJANA HANDSOME

KIJANA HANDSOME
Hakika duniani kuna viumbe mbalimbali, ebu tazama pozi hilo na jamaa alivyo, kweli Mungu anaviumbe vyake.

RATIBA KAMILI YA MKUTANO MKUU WA UCHUMI JUMAMOSI DON SUITE




RATIBA YA MKUTANO MKUU WA UWEKEZAJI. 9/01/2016 UTAKAO FANYIKA KTK UKUMBI WA DON SUITE HOTEL


SAA 5:00 MPAKA SAA 6:00 MCHANA.
Usomwaji wa taarifa ya manunuzi ya shamba la Fukayosi, na taarifa ya hali ya fedha katika account ya TPB. Pamoja na uwezekano wa kununua shamba jingine.

SAA 6 MPAKA SAA 7 MCHANA:
Majadiliano/Hatua za kufanya juu ya uanzishwaji wa Saccoss.

SAA 7 MPAKA SAA 7.45 CHAKULA CHA MCHANA.

SAA 7:45 MPAKA SAA 8:45. MCHANA.
Uanzishwaji wa  kampuni/ Uteuzi wa Board of Directors/ Mchanganuo wa ununuzi na umiliki wa share katika kampuni.

SAA 8:45 MPAKA SAA 9:00 ALASIRI MENGINEYO.

SAA 9:00 KUFUNGA MKUTANO.⁠⁠⁠⁠

BY DOLF GERLAD